Pata taarifa kuu
Sudan-Mapigano

Mapigano yaendelea kuchacha nchini Sudani Kusini

Mapigano yameendelea kushuhudiwa jana jumapili baina ya waasi wa Riek Machar na vikosi vya serikali ya Rais Salva Kiir ambapo kila uopande unadai kushikilia eneo la mapigano, baada ya kufeli kwa mazungumzo ya amani huko Nairobi nchini Kenya.

Mpiganaji mwanajeshi mtoto
Mpiganaji mwanajeshi mtoto
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na taarifa kutoka upande wa waasi, kiongozi wa kundi la waasi katika eneo la mapigano Johnson Olony ambae ni jenerali wa zamani katika jeshi la serikali kabla ya kujiunga na waasi mwezi Mei na ambae anatuhumiwa kuwaajiri watoto katika jeshi lake katika mji wa Malakal mji mkuu wa Jimbo la Hight Nile ndie ambae anashikilia mji huo, taarifa amabayo imekanushwa na serikali.

Wahudumu wa mashirika ya kibinadamu katika mji huo wamethibitisha kutokea kwa mapigano makali tangu siku ya Jumamosi katika mji jirani na mji wa mafuta ambao ndio pekee unaofanya kazi, umekuwa ukianguka mikononi mwa waasi kabla ya serikali kuurejesha kwa mara kadhaa.

Machafuko nchini Sudani Kusini yalianza tangu Desemba mwaka 2013 kati ya jeshi la serikali, na wanajeshi wanaomuunga Mkono aliekuwa makam wa rais wa zamani wa nchi hiyo Riek Machar na kuanzia mjini Juba mji mkuu kabla ya kutanda kote nchini.

Hakuna takwimu rasmi zilikwisha tolewa kutoka na mapigano hayo, lakini kulingana na waangalizi mamia ya watu wamepoteza maisha. Umaja wa Mataifa unasema, theluthi mbili ya wakazi milioni 12 wa nchi wanahitaji msaada ili kuendelea kuishi.

 

 

Hayo yanajir wakati kukiwa na taarifa kwamba Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na Kiongozi wa waasi Riek Machar, watakutana ana kwa ana kabla ya mwisho wa juma hili mjini Arusha, Tanzania kuweka sahihi katika mkataba wa kurejesha amani kwenye nchi hiyo changa barani Afrika.

Kukutana kwao kunatokana na shinikizo la Kenya na chama tawala nchini Tanzania chama cha Mapinduzi CCM

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.