Pata taarifa kuu
TUNISIA-JIHADI

Mawaziri wa 3 Ulaya wako nchini Tunisia kuungana na wananchi kulaani shambulio la kigaidi

Mawaziri kutoka nchi za Ulaya hii leo wameweka mashada ya maua kwenye fukwe ya bahari nchini Tunisia, ambako kulifanyika mauaji ya watu zaidi ya 38, baada ya mtu mmoja mwenye silaha kuwashambulia watu waliokuwepo kwenye fukwe hiyo. 

Picha zikionesha sehemu ya maua yaliyowekwa na waombolezaji nchini Tunisia.
Picha zikionesha sehemu ya maua yaliyowekwa na waombolezaji nchini Tunisia. REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mkuu wa Uingereza, asubuhi ya hii leo ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya kukabiliana na makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali, ikiwa ni pamoja na kuisaidia nchi ya Tunisia kukabiliana na ugaidi.

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Theresa May na waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere pamoja na waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve wamesafiri hadi nchini Tunisia kuungana na wananchi wa taifa hilo kuomboleza vifo vya raia hao.

Picha zaidi za tukio la Tunisia

Mawaziri hao wakiwa na mwenyeji wao waziri wa mambo ya ndani wa Tunisia, waliweka mashada ya maua kwenye fukwe ya hoteli ya Riu Imperial Marhaba ambako siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita ilishuhudia tukio baya la kigaidi.

Mauaji haya ambayo kundi la Islamic state limekiri kuhusika, ni shambulizi baya zaidi ya kijihadi kuwahi kutekelezwa katika historia ya nchi ya Tunisia na likiwa tukio baya zaidi kuwalenga raia wa Uingereza toka shambulio la bomu la mwaka 2005 jijini London.

Mamlaka nchini Tunisia, mpaka sasa wamefanikiwa kuwatambua watu 20 waliouawa kwenye tukio hilo ambapo kati yao 16 ni raia wa Uingereza, licha ya kuwa shirika la utangazaji la Uingereza limeripoti kuwa idadi hiyo huenda ikafikia 30.

Wakizungumza kwa pamoja mara baada ya kuweka mashada ya maua, waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza, Theresa May, amesema nchi yake inaungana na wananchi wa Tunisia katika kulaani shambulio hili, na kuongeza kuwa kama alivyosema waziri mkuu, David Cameron, nchi yake itaendelea kushirikiana na dunia pamoja na nchi ya Tunisia kuwakabili wapiganaji wa kijihadi.

Kwa upande wake, waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve, amesema kuwa nchi yake inalaani kwa nguvu zoet mauaji yaliyotekelezwa na mpiganaji wa kijihadi, na kwaba wako bega kwa bega na Tunisia katika kuhakikisha kuwa wapiganaji hawa wanadhibitiwa.

Hili ni shambulio jingine baya la kigaidi kutekelezwa nchini Tunisia katika kipindi cha miezi mitatu, kwani mwanzoni mwa mwaka hu, watu wenye silaha walishambulia watalii waliokuwa wakitembelea jumba la makumbusho la Tunisia.

Nchi ya Uingereza imetuma ndege yake ya kijeshi kwenda nchini Tunisia, kuwachukua manusura wengine wa ajali hiyo kwaajili ya matibabu zaidi.

Viongozi wote hawa kwa pamoja wameapa kuushinda ugaidi na kwamba hauna nafasi kwenye mataifa yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.