Pata taarifa kuu
CONGO-SASSOU-MAZUNGUMZO-SIASA

Congo: Sassou atangaza kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa

Baada ya kukutana kwa mazungumzo na wananchi 400 kati ya mwishoni mwa mwezi Mei na mwanzoni mwa mwezi Juni kuhusu mstakabali wa taifa la Congo, rais wa nchi hiyo Denis Sassou-Nguesso ametangaza Jumanne wiki hii kwenye runga ya taifa kwamba yuko mbioni kuitisha mazungumzo ya kitaifa.

Denis Sassou-Nguesso, hapa mjini akiwa Brussels Machi 3 mwaka 2015, alitangaza mara kadhaa uwezekano wa mageuzi ya Katiba, yatakayomruhusu kuwania muhula mwengine.
Denis Sassou-Nguesso, hapa mjini akiwa Brussels Machi 3 mwaka 2015, alitangaza mara kadhaa uwezekano wa mageuzi ya Katiba, yatakayomruhusu kuwania muhula mwengine. AFP PHOTO / THIERRY CHARLIER
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo hayo yanatazamiwa kuanza tarehe 11 hadi 15 Julai mwaka huu. Mazungumzo haya yatakua fursa ya kushughulikia masuala yanayohusiana na maandalizi ya uchaguzi ujao, ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa rais wa mwaka 2016, ambapo rais huyo anayemaliza muda wake haruhusiwi kikatiba kuwania muhula mwengine. Mustakabali wa taasisi pia utajadiliwa wakati wa mazungumzo hayo.

“ Nimeamua kuwa mazungumzo ya kitaifa yatafanyika kuanzia Juni 11 hadi 15 mwaka 2015 “, rais Sassou-Nguesso amesema katika hotuba fupi aliyoitoa kwenye runinga ya taifa.

Upinzani unamtuhumu rais Sassou-Nguesso kwamba ana nia ya kutaka kubadili Katiba ya nchi hiyo ili aweze kuwania muhula mwengine katika uchaguzi wa mwaka 2016.

Rais Denis Sassou-Nguesso amezungumzia kwa mapana pendekezo lake: “Nimeamua kuunda tume ya maandalizi ya mazungumzo ya kitaifa. Tume hiyo itaundwa na timu ya wataalam watakaohusika na kutoa majibu ya kiufundi kwa maswali yafuatayo: vipi tunapaswa kuandaa katika mazingira bora uchaguzi ujao nchini mwetu? Je, kuna haja ya kubadilisha au la taasisi za jamhuri? Kama ndiyo, kwa njia gani tunatakiwa kuendeleza taasisi hizo? Na kama sivyo, kwa nini? Washiriki watapewa nafasi ya kutoa majibu katika mazungumzo hayo", amesema rais Denis Sassou-Nguesso.

Hata hivyo hakueleza bayana ni vyama gani na watu wa waina gani ambao wataalikwa katika mazungumzo hayo. Upinzani, kwa upande wake ulisusia mkutano uliyoandaliwa na rais mwezi Mei na Juni wa kuandaa mazungumzo haya. Mpaka sasa upinzani haujaonesha nia yoyote ya kushiriki katika mazungumzo haya yanayotazamiwa kuanza Juni 11 hadi 15 mwaka 2015.

" Wakati huu sisi hatutalaumiwa kwamba hatukiitikia mwaliko wa rais wa Jamhuri. Kwa sababu tunahisi kwamba kila kitu tayari kimepangwa. Jana kuliitishwa vyama vya siasa, asasi mbalimbali kushiriki mkutano wa kiini macho. Lakini tulisema na tukasisitiza kuwa mpaka sasa taasisi zetu hazina tatizo. Tatizo hasa ni utawala wa uchaguzi, kwa hiyo mazungumzo yoyote yatakayojikita juu ya suala hili, tutashiriki. La sivyo hatutashiriki ", amesema Pascal Tsaty, Katibu wa kwanza wa chama kikuu cha upinzani UPADS.

Kwa upande wake rais wa Congo, Denis Sassou-Nguesso amesema “ mazungumzo yanaleta maaendeleo, maelewano na ufanisi”.

Sassou-Nguesso, mwenye umri wa miaka 72, yuko madarakani kwa kipindi cha miaka thelathini, lakini Katiba ya nchi ya Congo haimruhusu kuwania muhula mwengine. Hata hivyo aliwahi kubaini uwezekano wa kuitisha mazungumzo ya kitaifa kwa minajili ya kubadili baadhi ya vipengele vya Katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.