Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-BUNGE-UTAWALA-Siasa

Serikali ya Madagascar yakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu

Baada ya rais Hery Rajaonarimampianina mwezi mmoja uliyopita, Waziri mkuu Jean Ravelonarivo anaangaliwa kwa makini wakati huu. Wabunge wa Madagascar wamewasilisha barua ya kutokua na imani na serikali ya Madagascar, siku mbili kabla ya kumalizika kwa kikao cha bunge.

Jean Ravelonarivo, Waziri mkuu Madagascar, analengwa na uamzi wa kutokua imani na serikali yake uliyowasilishwa na zaidi ya wabunge mia moja. Uchaguzi utafanyika siku ya Ijumaa Julai 3.
Jean Ravelonarivo, Waziri mkuu Madagascar, analengwa na uamzi wa kutokua imani na serikali yake uliyowasilishwa na zaidi ya wabunge mia moja. Uchaguzi utafanyika siku ya Ijumaa Julai 3. AFP PHOTO / RIJASOLO
Matangazo ya kibiashara

Jaribio la mazungumzo lilianzishwa Jumatano mchana wiki hii kati ya wabunge na Ikulu ya rais, bila mafanikio. Uchaguzi utafanyika siku ya Ijumaa wiki hii.

Tishio la kutokua na imani dhidi ya serikali ya Waziri Mkuu Jean Ravelonarivo limekua likishuhudiwa kwa muda wa wiki kadhaa. Wabunge wa Madagascar hatimaye walisubiri mpaka dakika ya mwisho kuishambulia serikali, siku mbili kabla ya kumalizika kwa kikao cha bunge.

Waraka wa kutokua na imani dhidi ya serikali uliwasilishwa Jumatano wiki hii kwenye ofisi ya Bunge. Katiba inatoa muda wa masaa 48 kabla ya wabunge wote kupiga kura hiyo ya kutokua na imani. Waraka huo utapigiwa kura Ijumaa, Julai 3.

" Waziri Mkuu Jean Ravelonarivo hawezi kutatua matatizo ya kijamii na kiuchumi yanayoikabili nchi wakati huu ", Jean Brunelle Razafitsiandraofa ambaye ni mmoja wa wabunge waliotia saini kwenye waraka huo amebaini, huku akijaribu kuutetea uamzi huo dhidi ya serikali. Mgomo ambao unaoendelea kushuhudiwa, hususan mgogoro unaoendelea kulikumba shirika la ndege la Air Madagascar, kupanda kwa bei ya mafuta, ni miongoni mwa malalamiko yaliyowasilishwa kwa serikali.

Kura yapitishwa kwa wingi wa theluthi mbili

Ili uweze kupitishwa, uamzi wa kutokua na imani na serikali unapaswa kupigiwa kura wingi wa theluthi mbili ya wajumbe wa Bunge. Kundi la wabunge walioanzisha harakati hizo wamebaini kwamba zaidi ya wabunge mia moja kwa jumla ya 151 wametia saini kwenye waraka wa kutokua na imani dhidi ya serikali. Mei 26, wabunge hao ndio waliomuomba rais Herry Rajaonarimampianina ajiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.