Pata taarifa kuu
UFARANSA-ANGOLA-DIPLOMASIA

François Hollande awasili Angola

Rais wa Ufaransa François Hollande anaendelea na ziara yake barani Afrika. Baada ya Benin rais Hollande amewasili nchini Angola Alhamisi jioni wiki hii. Hollande anatazamia kuondoka nchini humo leo Ijumaa jioni.

rais wa Ufaransa, François Hollande, akiwasili katika mji wa Luanda, Angola, Julai 2 mwaka 2015.
rais wa Ufaransa, François Hollande, akiwasili katika mji wa Luanda, Angola, Julai 2 mwaka 2015. AFP PHOTO / ALAIN JOCARD
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo kati ya rais François Hollande na mwenyeji wake José Eduardo dos Santos yatajikita hasa katika sekta ya uchumi.

Mwaka jana, biashara kati ya Ufaransa na Angola iliongezeka kwa asilimia 70. Kuna soko la mafuta: Angola ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa mafuta barani Afrika, na Total ni kampuni ya kwanza katika soko hili.

Lakini siyo mafuta tu. Tangu bei ya mafuta ilipoanguka kwa kiwango cha asilimia 50 ya thamani yake, Angola imekua ikitafuta kuchanganya uchumi wake. François Hollande amewasili Alhamisi jioni katika mji mkuu wa Angola, Luanda akiambatana na baadhi zaidi ya viongozi hamsini wa makampuni ya Ufaransa ambao watashiriki leo Ijumaa asubuhi katika mkutano wa kiuchumi kati ya Ufaransa na Angola. Uchumi utapewa kipaumbelekatika mkutano huo.

Nchini Angola, rais José Eduardo dos Santos yuko madarakani kwa miaka 35 sasa. Wiki mbili zilizopita, wanaharakati kumi na tano wa mashrika ya kiraia, ikiwa ni pamoja na mwanamuziki wa miodoko ya Rap, Luaty Beirao, waliwekwa kizuizini kwa tuhuma za uasi. Bila hata hivyo kutaja Jose Marcos Mavungo, mwanaharakati wa haki za binadamu katika jimbo la Cabinda ambaye yuko kizuizini kwa zaidi ya miezi mitatu sasa. Lakini masuala yote haya yanachukiza na kuna uwezekano mdogo kuwa Hollande na mwenzake wa Angola wakayazungumzia.

Hata hivyo, nchini Benin, François Hollande alitoa hotuba ndefu ya zaidi ya dakika 25 ambapo alionesha msimamo wake wa kutounga mkono marais wanaobadili Katiba ili wasaliye madarakani.

Akiulizwa kwanini amekua akimkosoa rais wa Burundi kwa kunga'nga'nia madaraka kinyume cha sheria, wakati ambapo miongoni mwa nchi atakazotembelea kama Angola Cameroon na zinginezo kuna marais ambao wako madarakani kwa zaidi ya mihula miwili, rais Hollande amesema kuwa hotuba yake haijabadilika, na msimamo wa Ufaransa ni ule ule wa kutounga mkono marais wanaobadili katiba ili wasaliye madarakani. Hollande amesema demokrasia ni kupishana kwenye madaraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.