Pata taarifa kuu
BURUNDI-UCHAGUZI-SIASA

Burundi: chama cha rais chashinda viti 77 kwa jumla ya viti 100 Bungeni

Tume huru ya Uchaguzi nchini Burundi (Ceni) imetangaza Jumanne Julai 7 matokeo ya uchaguzi wa wabunge na madiwani uliofanyika Jumatatu Juni 29 mwaka huu.

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini Burundi, Pierre-Claver Ndayicariye.
Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini Burundi, Pierre-Claver Ndayicariye. DR
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume huru ya Uchaguzi (Ceni) chama tawala nchini Burundi (CNDD-FDD) kimeshinda viti 77 kwa jumla ya viti 100 vinavyohitajika katika Bunge la nchi hiyo katika uchaguzi ambao umeendelea kuzua utata kufuatia rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Muungano wa wagombea binafsi unaoongozwa na wapinzani Agathon Rwasa na Charles Nditije umejikuta umepewa viti 21. Muungano huo uliususia uchaguzi wa wabunge na madiwani uliyofanyika Juni 29, lakini umesema kushangazwa kuona unapewa kura hizo na Tume huru ya Uchaguzi (Ceni) wakati haukufanya kampeni za uchaguzi na ulitangaza wazi kwamba ulijiondoa katika uchaguzi huo.

Tume huru ya Uchaguzi (Ceni), kwa upande wake imebaini kwamba haujawahi kupokea barua rasmi ya kuomba kujiondoa kwa muungano huo (Amizero y'Abarundi) kwenye orodha ya wagombea.

Viti viwili vinavyosalia vimepewa chama cha Uprona kinachoshirikiana na chama tawala cha Cndd-Fdd.

Wakati huohuo katika mkutano uliyofanyika Jumatatu Julai 6 jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania, marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki waliamua kumteuwa rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni kuwa msuluhishi katika mgogoro wa Burundi.

Hayo yakijiri raia wa Burundi wameendelea kuitoroka nchi hiyo. Mpaka sasa zaidi ya wakimbizi 140,000 wamekimbilia katika mataifa jirani ya Tanzania, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.