Pata taarifa kuu
KENYA-SHABAB-MASHAMBULIZI-USALAMA

Kenya: watu 14 wauawa katika kijiji cha Soko Mbuzi

Nchini Kenya watu 14 wameuawa na zaidi ya 10 kujeruhiwa baada ya washukiwa wa kundi la Al Shabab kutoka nchini Somalia kuvamia kijiji cha Soko Mbuzi Karibu na mji wa Mandera, nchini Kenya.

Vikosi vya usalama vya Kenya sio tu kushindwa kulindia usalama wakazi dhidi Al Shabab, lakini pia kuhusika katika mauaji ya raia wakati wa operesheni zao.
Vikosi vya usalama vya Kenya sio tu kushindwa kulindia usalama wakazi dhidi Al Shabab, lakini pia kuhusika katika mauaji ya raia wakati wa operesheni zao. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hili limethibitishwa na Kamishena wa Kaunti ya Mandera Alex Ole Nkoyo ambaye amesema wanamgambo hao walivamia kijiji hicho saa saba usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne wiki hii.

Washambuliaji hao walitumia maguruneti na bastola kuwalenga watu waliokuwa wanalala kwenye mahema nje ya nyumba zao kutokana na joto kubwa katika eneo hilo.

Makabiliano makali kati ya vyombo vya usalama na wanamgambo wa Al Shabab yalitokea Jumatatu usiku Mei 25, Kaskazini Magharibi mwa Kenya. Kijiji cha Yumbis na maeneo mengine yaliyopembezoni katika Kaunti ya Garissa, yalilengwa na wanamgambo hao wa Al Shabab.

Kenya imekua ikilengwa na mashambulizi ya Al Shabab, baada tu nchi hiyo kuchukua uamzi wa kuwatuma wanajeshi wake kujiunga na kikosi cha Umoja wa Afrika kusimamia amnai nchini Somalia.

Hata hivyo serikali ya Kenya imeapa kutowaondoa wanajeshi wake nchini Somalia, licha ya vitisho na mashambulio hayo yanayotekelezwa na Al Shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.