Pata taarifa kuu
KENYA-OBAMA-DIPLOMASIA

Kenya: Ulinzi waimarishwa Nairobi kwa ajili ya mapokezi ya Obama

Mji wa Nairobi umekua msafi kwa ajili ya kuwasili kwa Barack Obama Ijumaa usiku. Wakaazi wa Nairobi wanaona kwa sasa muda unayoyoma. Rais wa Marekani atafanya masaa 48 katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kabla ya kujielekeza nchini Ethiopia.

Barack Obama atakaa siku mbili Nairobi, mji mkuu wa Kenya.
Barack Obama atakaa siku mbili Nairobi, mji mkuu wa Kenya. AFP PHOTO / SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Ziara yake nchini Kenya itaongozana na hatua nane kwa kuyatembelea maeno zaidi ya kumi ambayo yatakau kama maeneo ya heshima kwa rais wa 44 wa Marekani.
Serikali ya Kenya imeimarisha ulinzi katika mji wa Nairobi, hasa katika maeneo ambayo rais wa Marekani atatembelea, ikiwa ni pamoja na Chuo kikuu cha Kentatta.

Wakati huo huo shirika linalosimamia safari za ndege nchini Kenya, KCAA, limetangaza kuwa anga ya Kenya itafungwa kwa muda wa dakika hamsini siku ya Ijumaa wiki hii ili kuruhusu ndege ya rais wa Marekani Barrack Obama kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.

Rais wa Marekani Barack Obama anatazamiwa kuwasili mjini Nairobi siku ya Ijumaa Julai 24, na rais wa Kenya Jumanne wiki hii alielezea matarajio yake kwa ajili ya ziara ya Barack Obama nchini mwake.

Biashara na mapambano dhidi ya ugaidi ni mada mbili ambazo zitapewa kipaumbele, amesema Uhuru Kenyatta. Rais huyo amepuuzia athari za uhalifu wa kivita uliyokua ukimkabili. Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imeahirisha kesi yake kwa muda usiojulikana kwa kukosa ushahidi. Kwa sasa ziara ya Obama inakuja kusaiadia kurejesha sifa za rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Wakati wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2013, mwanadiplomasia mmoja wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika wa wakati huo alijaribu kukatisha tamaa wapiga kura wa Kenya kutowapigia kura Uhuru Kenyatta William Ruto. Wawili hao leo ni viongozi vigogo nchini Kenya. Rais wa Kenya na Makamu wa wake walikua walifunguliwa mashitaka na ICC kwa kuhusika kwao katika ghasia ziliyofuata uchaguzi wa mwaka 2007.

Lakini ukurasa huo umebadilika, alisema Uhuru Kenyatta Jumanne wiki hii. "Hakuna kitu kinachozikutanisha nchi zetu hizi mbili ispokua maadili ambayo tunachangia. Na wale wote ambao wameonyesha mashaka juu ya uewezekano wa ushirikiano na urafiki kati ya nchi zetu mbili wangelirejelea uchambuzi wao", ameonya rais wa Kenya.

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu ICC ilifuta mashtaka dhidi ya Uhuru Kenyatta mwezi Desemba mwaka 2014 kwa kukosa ushahidi, lakini makamu wake William Ruto, hajafutiwa mashtaka. Hii haitazuia kupeana mikono kati ya Obama na William Ruto, amesema rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. Mada hii imekua gumzo nchini Kenya. " Hakuna shaka kwamba Obama anakuja kukutana na serikali iliopo madarakani, ni kusema wajumbe wote wa serikali, kwa sasa hili suala halina nafasi wakati huu, kwani makamu wa rais ni mmoja wa wajumbe wa serikali hii, hivyo tutaweza kukutana sote na kinachohitajika wakati huu ni ushirikiano kati ya Kenya na Marekani ", amesema Uhuru Kenyatta.

Ulinzi nchini Kenya umeimarishwa ikisalia siku moja tu kabla ya kuwasili kwa rais wa Marekani Barack Obama. Mpaka sasa haijajulikana iwapo Obama atatembelea kijiji cha Kogelo alikozailwa baba yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.