Pata taarifa kuu
BURUNDI-AU-USHIRIKIANO-USALAMA

Wataalam wa Umoja wa Afrika wapelekwa Burundi

Wataalam wa Umoja wa Afrika wameanza kupelekwa nchini Burundi Tangu Jumatano wiki hii. Wataalam hawa wa kijeshi na wa haki za binadamu walitumwa hasa na Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika mwezi Juni.

Askari polisi katika mtaa mmoja wa Bujumbura, Julai 6 mwaka 2015.
Askari polisi katika mtaa mmoja wa Bujumbura, Julai 6 mwaka 2015. AFP PHOTO / Landry NSHIMIYE
Matangazo ya kibiashara

Lengo la kutumwa kwa wataalam hawa ni kuchunguza na kusimamia zoezi la kupokonya silaha raia wanao zimiliki pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu. Lakini zoezi la kutumwa kwa wataalam hao limechelewa mwezi mmoja ili lianze, lakini litaendeshwa kwa hatua.

Marekani imeishtumu serikali ya Burundi kuwa ilifanya kilio chini ya uwezo wake ili kuzuia kupelekwa kwa wataalam hao kabla ya uchaguzi wa urais wa Julai 21.

Mwezi mmoja baada ya uamuzi huo, hakuna kundi hata moja la wataalam ambalo limekua limeshatumwa nchini Burundi. Umoja wa Afrika uliamua kutoa tangazo Jumamosi ili kueleza changamoto zilizosababisha zoezi hilo kuchelewa. Pamoja na mambo mengine serikali ya Burundi ilipendekeza tarehe ya kutumwa kwa wataalam hao baada ya Julai 15, siku hiyo ndio ilikua ilipangwa kufanyika uchaguzi wa urais, kabla ya kuahirishwa hadi Julai 21. Siku tatu baada ya tangazo hili, Marekani ilimtuhumu moja kwa moja waziri wa mambo ya nje wa Burundi kuwa alifanya kilio chini ya uwezo wake ili kuchelewesha kuwasili kwa wataalam hawa.

Alain Aimé Nyamitwe amekanusha tuhuma hizo za Marekani: " Tulishirikiana moja kwa moja na Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika. Kulikuwa na heka heka, na jambo hilo halikutokana na serikali ya Burundi pekee. Kulikuwa na ahadi ya kupelekwa kwa tume hizi mbili mapema iwezekanavyo, lakini kila upande unatafsiri jinsi unavyoelewa neno hili: mapema iwezekanavyo, ikiwa ni upande wetu au upande wa Umoja wa Afrika. Sisi tuliomba tuweza kufanya kazi pamoja ili tuweze kuzipa tume hizi muongozo mzuri ", amesema waziri wa mambo ya nje wa Burundi.

Hata hivyo hali ya wasiwasi imeendelea kutanda nchini Burundi, siku mbili baada ya uchaguzi wa urais. Raia wamekua na hofu ya kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, baada ya baadhi ya wanajeshi kuendelea kuitoroka nchi na kuelekea sehemu isiyojulikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.