Pata taarifa kuu
MAREKANI-KENYA-DIPLOMASIA-USALAMA-UGAIDI

Barack Obama ziarani Kenya

Ndege ya Barack Obama inatazamiwa kutua leo Ijumaa jioni mjini Nairobi. Wakenya wamekua wakijiandalia kwa muda mrefu ziara hii ya kihistoria. Rais wa Marekani anatembelea kwa mara ya kwanza nchi ya mababu zake. Ulinzi mkali umeimarishwa kwa sababu ya tishio la kundi la Al Shebab bado limetanda nchini Kenya.

Mhudumu wa mgahawa mmoja wa Nairobi akifanya usafi, huku akiosha vio kwa ajili ya mapokezi ya rais wa Marekani, Julai 23 mwaka 2015.
Mhudumu wa mgahawa mmoja wa Nairobi akifanya usafi, huku akiosha vio kwa ajili ya mapokezi ya rais wa Marekani, Julai 23 mwaka 2015. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya ulinzi vya Kenya vimekua vikipiga doria katika mji wa Nairobi huku wanajeshi wengine wakiwekwa katika maeneo muhimu, hasa mbele hoteli za kifahari. Mara kwa mara, vifaa vya Marekani nusu helikopta au nusu ndege vimekua vikizunguka kwenye anga ya mji wa Nairobi na vitongoji vyake. Vikosi vya usalama vimewekwa katika maeneo mbalimbali, na barabara kuu zitakuwa zimefungwa kwenye majira ya jioni leo Ijuma.

Nchini Kenya, ziara ya rais Barack Obama imegonga vichwa vya habari kwa muda wa zaidi ya siku kumi na watu wamwkua wakitoa maoni yao kuhusu ziara hiyo. Lakini ukubwa wa kazi inayofanyika ya kuupamba mji wa Nairobi, hatua za usalama, ikiwa ni pamoja na ukaguzi katika mitandao ya kijamii, vimeendelea kushuhudiwa katika mji huo.

Mji wa Nairobi umekua msafi kwa ajili ya kuwasili kwa Barack Obama. Rais wa Marekani atafanya masaa 48 katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kabla ya kujielekeza nchini Ethiopia.

Ziara ya rais wa Marekani nchini Kenya itaongozana na hatua nane kwa kuyatembelea maeno zaidi ya kumi ambayo yatakua kama maeneo ya heshima kwa rais wa 44 wa Marekani.
Serikali ya Kenya imeimarisha ulinzi katika mji wa Nairobi, hasa katika maeneo ambayo rais wa Marekani atatembelea, ikiwa ni pamoja na Chuo kikuu cha Kentatta.

Wakati huo huo shirika linalosimamia safari za ndege nchini Kenya, KCAA, limetangaza kuwa anga ya Kenya itafungwa kwa muda wa dakika hamsini siku ya Ijumaa wiki hii ili kuruhusu ndege ya rais wa Marekani Barrack Obama kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.

Jumanne wiki hii rais wa Kenya alielezea matarajio yake kwa ajili ya ziara ya Barack Obama nchini mwake.

Biashara na mapambano dhidi ya ugaidi ni mada mbili ambazo zitapewa kipaumbele, amesema Uhuru Kenyatta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.