Pata taarifa kuu
BURUNDI-EU-MSAADA-USALAMA-SIASA

EU yatathmini kusitisha moja kwa moja msaada Burundi

Umoja wa Ulaya EU umeanza kikao maalum kujadili uwezekano wa kusitisha moja kwa moja msaada wake nchini Burundi. Inasadikiwa kuwa fedha kutoka Umoja huo zinakadiria kufikia asilimia zaidi ya 50 ya bajeti nzima ya kila mwaka ta taifa hilo ndogo la Afrika ya Kati.

Wapinzani dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza wakiandamana Bujumbura, Juni 4 mwaka 2015.
Wapinzani dhidi ya muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza wakiandamana Bujumbura, Juni 4 mwaka 2015. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa masuala ya kigeni wa Umoj wa Ulaya Federica Mogherini, amsema kutiwa wasiwasi juu ya ya machafuko yaliyotokea nchini humo kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais Julai 21, na amesema ana mashaka kuwa huwenda serikali itakayoundwa baada ya uchaguzi huo isiwatendei haki raia wote wa taifa hilo.

Upinzani ulisusia uchaguzi huo wa urais hata ule wa wambunge na madiwani uliofanyika Juni 19. Vyama vikuu vya upinzani na mashirika ya kiraia vinapinga muhula wa tatu wa rais Nkurunziza, vikibaini kwamba ni kinyume na Katiba ya nchi na Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha.

Marekani na Umoja wa Ulaya zimeendelea kuonyesha kuwa uamuzi wa rais Pierre Nkurunzinza kuwania urais kwa muhula wa tatu ni kinyume na mkataba waliosaini mjini Arusha mwezi Agosti mwaka 2000, ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe viliodumu aidi ya mwongo mmoja.

Zaidi ya watu 80 wameuawa tangu kuzuka kwa machafuko nchini Burundi kufuatia maandamano ya kupinga muhula watatu wa rais Pierre Nkurunziza. Polisi na vijana kutoka chama madarakani Cndd-Fdd, Imbonerakure wameendelea wkunyooshewa kidole cha lawama kwamba walihusika katika mauaji hayo. Hata hivyo serikali imekua ikituhumu vyama vikuu vuya upinzani na mashirika ya kiraia kuchochea vurugu hizo, ambazo ilizitaja kuwa na lengo la kuzipindua taasisi za nchi ziliyochaguliwa na raia.

Wakti huu raia wameendelea kuwa na hofu ya kutokea kwa vita baada ya wanajeshi kadhaa kuendelea kuitoroka nchi na kukisiwa kuwa wamekua wakijiunga na makundi ya waasi ambao wanalenga kuanzisha vita dhidi ya utawala wa Nkurunziza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.