Pata taarifa kuu
KENYA-MAREKANI

Raisi wa Marekani Barack Obama kuongoza mkutano wa wajasiriamali Nairobi

Rais wa Marekani Barack Obama ambaye alikuwa akisubiriwa kwa hamu nchini Kenya amewasili jijini Nairobi usiku waijumaa na kulakiwa na rais wa Kenya uhuru Kenyatta tayari kwa kuongoza kongamano la kimataifa kuhusu uwekezaji na ujasiriamali kongamano ambalo litahudhuriwa na wajumbe wapatao elfu tatu ambao ni wawekezaji na wajasiri mali.

Raisi wa Marekani Barack Obama mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa JKIA jijini Nairobi jana
Raisi wa Marekani Barack Obama mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa JKIA jijini Nairobi jana REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Kando na hayo kiongozi huyo wa Marekani anatarajiwa kuzungumzia harakati za kupambana na ugaidi na haki za binadamu katika ziara yake ya kwanza katika taifa hilo tangu kuingia madarakani.

Ulinzi na usalama umeimarishwa vilivyo jijini Nairobi huku kukishuhudiwa baadhi ya barabara na safari za anga zikizuiwa hadi kutamatika kwa ziara hiyo.

Kuimarishwa kwa usalama mjini Nairobi ni kufuatia tishio la mashambulizi ya kigaidi ambayo hutekelezwa na wanamgambo wa Alshabab ambao wamekuwa wakitekeleza mauaji nchini humo likikumbukwa shambulizi katika chuo kikuu cha Garisa mnamo mwezi April na kuua wanafunzi zaidi ya ia moja.

Ziara ya raisi Obama nchini kenya inatarajiwa kumalizika jumapili ambapo ataondoka na kuelekea nchini Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.