Pata taarifa kuu
BURUNDI-AU-USHIRIKIANO-USALAMA

Burundi: wataalam wa AU waruhusiwa kuendesha kazi yao

Zaidi ya waangalizi kumi kutoka Tume ya haki za binadamu na wataalam wa kijeshi wa Umoja wa Afrika, waliowasili nchini Burundi wiki iliyopita hatimaye wameruhusiwa kupiga kambi yao nchini humo baada ya kupokelewa na wizara ya mambo ya Nje ya Burundi.

Ilibidi kusubiri uchaguzi wa Pierre Nkurunziza, baada ya uchaguziwa huo wa Julai 21 unaoendelea kuleta utata, ili serikali ya Burundi iruhusu wataalamu wa Umoja wa Afrika kuingia nchini humo.
Ilibidi kusubiri uchaguzi wa Pierre Nkurunziza, baada ya uchaguziwa huo wa Julai 21 unaoendelea kuleta utata, ili serikali ya Burundi iruhusu wataalamu wa Umoja wa Afrika kuingia nchini humo. PHOTO / PHIL MOORE
Matangazo ya kibiashara

Munamo tarehe 13 Juni mwaka huu, Tume ya Amani na Usalama ya Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika mjini Johannesburg limeazimia kusaidia nchi ya Burundi kujikwamua na mgogoro wa kisiasa kufuatia uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kugombea awamu, hatua ambayo imekumbana na maandalizi ya uchaguzi kama anavyobainisha Thomas BARANKITSE, Msaidizi wa Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Burundi.

 “ Haikua rahisi ”, kwa mujibu wa vyanzo kweny Umoja wa Afrika. Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika lililokutana Juni 13 mjini Johannesburg, lilipendekeza kutuma wataalam nchini Burundi ndani ya wiki mbili, lakini viongozi wa Burundi hawakuchelewa kuwazuia.

Serikali ya Burundi ilifanya kilio chini ya uwezo wake ili kuzuia timu hiyo ya wataalam wa Umoja wa Afrika kuwasili mapema mjini Bujumbura, kabla ya uchaguzi wa urais uliofayika Julai 21.

Lakini mwakilishi wa waziri wa mambo ya nje, Thomas Barankitse, ambaye aliwapokea wataalam hao, amezinyooshea kidole cha lawama taasisi za Umpja wa Afrika kuchelewa kutoa ratiba na programe ya timu hiyo nchini Burundi.

Umoja wa afrika ilitaka kuwatuma waangalizi 70 wa haki za binadamu na wataalam wa kijeshi. Serikali ya Burundi ilitupilia mbali idadi hiyo na kukubali 15 kwa kila timu. Kwa sasa ni vigumu kwa timu hizi kutekeleza kazi yao katika mazingira kama hayo kwa muda muafaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.