Pata taarifa kuu
NIGERIA-CAMEROON-BENIN-NIGER-CHAD-BOKO HARAM-USALAMA

Kikosi cha kimataifa kiko mbioni kupambana dhidi ya Boko Haram

Nigeria imemteua Generali mpya kuongoza kikosi cha kimataifa kilichoundwa kwa ajili ya kupamba dhidi ya kundi la wanamgambo wa kundi la Islamic State katika Afrika magharibi (Boko Haram).

Ofisi kikosi cha kimataifa kitakachopambana dhidi ya Boko Haram ziko katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena.
Ofisi kikosi cha kimataifa kitakachopambana dhidi ya Boko Haram ziko katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena. REUTERS/Moumine Ngarmbassa
Matangazo ya kibiashara

Meja General Iliyasu Isah Abbah ataongoza kikosi hiki kitakachokuwa na wanajeshi takriban 8500 ikiwa ni pamoja na askari polisi 2000 kutoka nchi tano.

Nigeria imemchagua General huyo mpya kwa lengo la kupambana na wanamgambo hao wa kundi la kigaidi la Boko Haram.

Uongozi wa kikosi hiki cha kimataifa umekamilika. Uongozi wa kikosi hiki unaundwa kwa sasa na jenerali mmoja kutoka Nigeria, mkuu wa majeshi kutoka Chad na afisa mwengine wa jeshi kutoka Cameroon. Dhana ya uendeshaji na sheria za ushiriki zilipitishwa miezi kadhaa iliopita.

Kikosi hiki kinatarajiwa kuwa na ofisi zake katika mji mkuu wa Chad N'Djamena na kinatarajiwa kuendesha operesheni zake kikamilifu kuanzia mwezi ujao.

Nigeria na majirani zake wamekuwa wanajitahidi kupambana na wapiganaji wa Boko Haram ambao wameua watu wzaidi ya elfu ishirini katika Ukanda huo wa Afrika Magharibi.

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa umetolea wito wiki hii jumuiya ya kimataifa kuzitolea msaada wa kifedhanchi za Nigeria, Cameroon, Chad, Niger na Benin, nchi ambazo zinachangia kwa kikosi hiki chenye lengo la kupambana na kundi la Islamic State katika Afrika magharibi (Boko Haram).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.