Pata taarifa kuu
DRC-HAKI-SHERIA

Wanajeshi wawatu wa DRC wako mbioni kufunguliwa mashitaka

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itawafungulia mashtaka askari wake watatu waliotuhumiwa kwa ubakaji nchini Jamhuri ya Afrika ya kati ambao ni sehemu ya ujumbe wa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kijiji cha Aveba.
Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kijiji cha Aveba. Photo MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo imetolewa Alhamisi wiki hii na waziri wa sheria wa Congo, Alexis Thambwe Mwamba, akibainisha kuwa tayari amemuagiza Jenerali [Joseph] Ponde, mwendesha mashtaka mkuu wa vikosi vya kijeshi nchini humo kufungua mashitaka hayo kulingana na msingi wa madai ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumza na shirika la habari la Ufaransa AFP, Alexis Tambwe mwamba ameongeza kuwa DRC haitaweza "kuvumilia" vitendo kama hivyo, na kwamba askari waliohusika watalazimika kurejeshwa nchini humo kukabiliana na mahakama ya kijeshi.

Imeripotiwa kwamba wanawake watatu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wamebakwa na askari watatu wa Congo, mdogo wao akiwa na umri wa miaka 15, huku wakishinikizwa kutotoa siri, huku mwingine akidaiwa tayari kuwa mjamzito wakati mwingine akikiri kuridhia uhusiano huo.

Jeshi la DRC ndilo pekee lina askari wake mjini Bambari ambapo matukio hayo yanaripotiwa na ambako hivi karibuni, ujumbe wake unatarajiwa kuwasili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuchunguza tuhuma hizo zinazodaiwa na kikosi cha Congo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwa ni njama na uongo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.