Wazazi wa Reeva Steenkamp wamshushia lawama Oscar Pistorius
Wazazi wa Reeva Steenkamp wanasema mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius alimpiga risasi na kumuua binti yao kwa makusudi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Wazazi wa Steenkamp wameimbia Runinga ya Australia maisha yao yamekuwa magumu na hawako tayari kuzungumza na Pistorius.
Wakitoa kauli hiyo kwa mara ya kwanza tangu kutolewa kwa hukumu ya Pistorius mwaka jana aliyehukumiwa jela kwa miezi kumi kwa kosa la kuua bila kukusudia na alitarajiwa kuachiliwa huru wiki iliyopita lakini Waziri wa haki Michael Masutha akabadilisha hatua hiyo.
Wazazi hao wamesisitiza kuwa uamuzi uliofanywa na Mahakama haukuwa sahihi.
Viongozi wa Mashtaka wiki iliyopita waliwalisha rufaa ya kutaka uamuzi wa Mahakama mwaka uliopita ubadilishwe na kumhukumu Pistorius kwa kosa la kuua kwa kukusudia.
Ikiwa uamuzi wa Mahakama iliyompa hukumu hiyo utabadilishwa huenda akafungwa jela miaka 15.