Serikali mpya ya Burundi yaundwa
Hatimaye rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ameunda serikali mpya yenye mawaziri ishirini, licha ya kuendelea kutengwa kimataifa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Baraza hili jipya la mawaziri linaundwa na washirika wa karibu wa rais huyo, wengi wao ni wale waliohudumu katika mihula miwili iliopita.
Wizara muhimu zimepewa washirika wake wa karibu.
Alain Aimé Nyamitwe, kaka wa mshauri mkuu wa rais Nkurunziza, anayehusika na mawasiliano, ameteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.
#Burundi Ministre de l'Interieur et de la Formation Patriotique: Mr Pascal Barandagiye
— Burundi | Présidence (@BdiPresidence) August 24, 2015
#Burundi Ministre de la Sécurité Publique: Commissaire de Police Chef Allain Guillaume Bunyoni
— Burundi | Présidence (@BdiPresidence) August 24, 2015
Pascal Barandagiye, aliyekuwa waziri wa sheria tangu mwaka 2010 hadi mwaka huu ameteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani.
Alain Guillaume Bunyoni, aliyekuwa kipndi fulani waziri wa usalama na baadaye afisa anayehusika na safari za rais, ameteuliwa kuwa waziri wa usalama.
Waziri wa zamani wa ulinzi Emmanuel Ntahomvukiye, aliyeteuliwa hivi karibuni baada ya jenerali Pontien Gaciyubwenge kuachishwa kazi kwenye wadhifa huo, ameendelea kushikilia wadhifa wake.
Waziri wa zamani wa mambo ya jumuiya ya Afrika Mashariki, Léontine Nzeyimana, ameendelea kushikilia wadhifa wake.
Waziri wa zamani wa sheria baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, Aimée Laurentine Kanyana, amerejeshwa kwenye wadhifa wake.
Waziri wa zamani wa fedha, Tabu Abdallah Manirakiza, ameendelea kushikilia wadhifa wake.
Janvière Ndirahisha, ameteuliwa kuwa waziri wa elimu ya msingi, sekondari, elimu ya juu na utafiti wa sayansi.
Déo Guide Rurema, ameteuliwa kuwa waziri wa kilimo na mifugo.
Nestor Bankumukunzi, ameteuliwa kuwa waziri wa posta, mawasiliano na teknolojia ya habari.
Emmanuel Niyonkuru, ameteuliwa kuwa waziri wa maji, mazingira na ujenzi wa miji.
Pélate Niyonkuru, ameteuliwa kuwa waziri wa biashara.
Josiane Nijimbere, ameteuliwa kuwa waziri wa afya.
Côme Manirakiza, ameteuliwa kuwa waziri wa nishati na madini
Serges Ndayiragije, waziri wa utawala bora.
Félix Mpozerirenga, waziri wa wafanyakazi, kazi na ajira
Jean Bosco Ntunzwenimana, waziri wa uchukuzi
Jeanne d’Arc Kagayo, waziri wa maendeleo ya wilaya
Waziri wa zamani wa utawala bora, Martin Nivyabandi, ameteuliwa kuwa waziri wa haki za binadamu, jamii, na jinsia
Jean Bosco Hitimana, ameteuliwa kuwa waziri wa vijana, michezo na utamaduni