Pata taarifa kuu
RIADHA-KENYA-CHINA-MCHEZO

Riadha: Kenya yaendelea kufanya vizuri Beijing

Wakenya wameendelea kupata medali katika mashindano ya Riadha ya dunia yanayoendelea jijini Beijing nchini China.

Mwanariadha wa Kenya, Julian Yego.
Mwanariadha wa Kenya, Julian Yego. REUTERS/Kai Pfaffenbach
Matangazo ya kibiashara

Julius Yego ameweka historia kwa kuwa Mkenya wa kwanza kushinda dhahabu katika urushaji mkuki na alirusha kwa umbali wa Mita 92.72 na kumshinda Ihab Abdelrahman El Sayed kutoka Misri aliyeibuka katika nafasi ya pili na Tero Pitkamaki akimaliza wa tatu.

Yego alianza mchezo wa urushaji mkuki kwa kuangalia video kupitia Yutube.

Mbali na Yego, Mkenya mwingine Hyvin Kiyeng Jepkemoi amenyakua dhahabu katika mbio za mita elfu tatu kuruka viunzi na maji, mbio alizomaliza kwa muda wa dakika 9 sekunde 19 nukta 11.

Kwa matokeo ya leo, Kenya wanaendelea kuongoza jedwali la Medali kwa medali 11, sita za dhahabu, tatu za fedha na 2 za shaba.

Uingereza na Jamaica ni za pili kwa medali tatu.

Lakini pia Jumatano wiki hii ilikuwa ni siku yenye huzuni kwa wanariadha wawili wa Kenya Koki Manunga ana Joyce Zakary wanaokimbia mbio fupi za Mita 400 kwa upande wa wanawake baada ya kubainika kuwa walikuwa wanatumia dawa za kuwaongeza nguvu mwilini.

Shirikisho la riadha duniani limetangaza kuwa limewapiga marufu ya kushiriki katika mashindano haya ya dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.