Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA-USALAMA

Kuanza kwa mazungumzo imekuwa vigumu Burundi

Nchini Burundi, upinzani unasema kwamba haumtambui Pierre Nkurunziza kama rais wa nchi hiyo tangu Jumatano, Agosti 26, siku ya mwisho ya muhula wake wa pili.

Rais Pierre Nkurunziza, Agosti 20, 2015.
Rais Pierre Nkurunziza, Agosti 20, 2015. AFP PHOTO / LANDRY NSHIMIYE
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanathibitishwa na Cnared, jukwaa la kisiasa linaloundwa na wafuasi wa zamani wa chama chake Pierre Nkurunziza, vyama vikuu vya upinzani na vyama vya kiraia.

Wakati huo huo, mjini Bujumbura, Jumatano wiki hii Pierre Nkurunziza, aliwahutubia wananchi kwa mara ya kwanza tangu aapishwe kuchukua madaraka kwa muhula wa tatu, hotuba ambayo iligubikwa na suala la usalama. Hayo yakijiri baraza la mawaziri limefanya kikao chake cha kwanza Jumatano wiki hii. Hali hiyo huenda ikazua machafuko.

Jumuiya ya kimataifa ina hofu ya kutokea kwa machafuko nchini Burundi, na ina mashaka ya kutokuwepo tena kwa mazungumzo kati ya serikali na wadau wote wanaopinga muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza.

Baadhi ya wanadiplomasia wa kigeni nchini Burundi wanaona kwamba serikali utawala mpya wa Nkurunziza, licha ya kutotambuliwa kimataifa, unataka kutumia nguvu kwa kuwatia uoga raia ili kujitenga na mazungumzo na kufanya kile inachokitaka.

Miongoni mwa hatua zinazowatia hofu wanadiplomasia mjini Bujumbura ni pamoja na marekebisho ya sheria ihusuyo mashirika yasio ya kiserikali, hadhi ya vyama vya kiraia na madhehebu ya dini. Baadhi ya vyama vya kiraia vilikuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya awamu ya tatu ya Pierre Nkurunziza.

Agathon Rwasa na Pascal Nyabenda mjini Kampala

Mapema wiki hii, katika duru za kidiplomasia, kwa mara nyingine tena zilionyesha kurudi mjini Bujumbura kwa mpatanishi wa Uganda kwa ajili ya mashauriano na kuanza upya kwa mazungumzo yaliositishwa kabla ya uchaguzi wa urais. Hata hivyo inaonekana kuwa hakuna uwezekano wa kuanza kwa mazungumzo hayo. Lakini sasa, kwa mshangao wa kila mtu, Spika wa Bunge akiwa pia kiongozi wa chama tawala, Pascal Nyabenda, na naibu wake wa kwanza Agathon Rwasa, wametumwa katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, wakati ambapo wafuasi wa tano wa Agathon Rwasa aliyekua akipinga na kususia uchaguzi huo wameteuliwa kuwa mawaziri wa serikali hiyo mpya, aliyoipinga tangu awali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.