Pata taarifa kuu
KENYA-ICC-SHERIA-HAKI

Baadhi ya wabunge wa Kenya wamtaka William Ruto kukaidi amri ya ICC

Sakata la kesi inayomkabili naibu wa rais nchini Kenya, William Ruto katika Mahakama ya kimataifa ya ICC, limechukua sura mpya kufuatia baadhi ya wabunge wa chama tawala nchini humo kumtaka kiongozi wao kukaidi amri ya mahakama ya ICC.

Naibu wa rais wa Kenya, William Ruto akiwa kwenye mahakama ya ICC kujibu mashtaka ya uhalifu wa kibanadamu inayomkabili
Naibu wa rais wa Kenya, William Ruto akiwa kwenye mahakama ya ICC kujibu mashtaka ya uhalifu wa kibanadamu inayomkabili Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wabunge hao wanadai kuwa mahakama hiyo imegeuka kuwa ya kisiasa na sio ya kisheria tena, baada ya uamuzi wa juma moja lililopita, Majaji waliporuhusu kiongozi wa mashtaka kutumia ushahidi wa mashahidi waliojiondoa kwenye kesi ya Ruto lakini ushahidi wao ulirekodiwa.

Wakili wa Ruto, Karim Khan amewasilisha pingamizi lake kwenye mahakama akisisitiza kuwa uamuzi wa jopo la majaji wa rufaa umeenda kinyume na haki za watuhumiwa.

Akizungumza Jumapili, mwishoni mwa juma hili lililopita, naibu wa rais William Ruto amesisitiza utayari wake wa kuendelea kushirikiana na mahakama hiyo.

Wakati hayo yakijiri muhula mpya wa shule unaanza leo Jumatatu nchini Kenya, na huenda wanafunzi walioanza kuripoti shuleni toka mwishoni mwa juma lililopita, wasianze kusoma kwa wakati, kufuatia tangazo la chama cha waalimu nchini humo KNUT kuwataka waalimu kutorejea kazini mpaka madai yao ya kuongezewa mshara kati ya asilimia 50 hadi 60 kutekelezwa .

Jumapili Agosti 31, kupitia taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari, tume ya kuajiri waalimu nchini Kenya TSC, imewaagiza walimu zaidi ya laki mbili kurejea kazini kuanzia leo Jumatatu bila kukosa, huku ikisisitiza kuwa haijapokea barua yoyote kutoka chama cha waalimu kueleza kuanza kwa mgomo huo.

Hata hivyo viongozi wa waalimu wanasisitiza kuwa wanachama wao hawatarejea kazini hadi pale nyongeza yao ya mshahara ilio kati ya asilimia 50 na 60 utakapolipwa na serikali.

Sintofahamu hii inajiri ikiwa ni juma moja tu, toka mahakama ya Juu nchini humo, itupilie mbali rufaa ya tume ya kuajiri walimu kupinga nyongeza ya mshahara wa waalimu.

Katibu Mkuu wa KNUT, Wilson Sossion, amesisitiza kuhusu mgomo wao.

Serikali imewasilisha kesi nyingine katika Mahakama ya rufaa kupinga nyongeza hii ya mshahara, huku ikisisitiza kuwa kwa sasa haikutenga fungo lolote la fedha kuwalipa waalimu hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.