Pata taarifa kuu
MISRI-UCHAGUZI-SIASA

Misri yajiandalia uchaguzi wa wabunge

Misri imetangaza uchaguzi wa wabunge utafanyika kwa hatua mbili mwezi wa Oktoba na Novemba mwaka huu.

Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sissi, baada ya mkutano na baraza la majeshi, Jumamosi Aprili 4 Cairo.
Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sissi, baada ya mkutano na baraza la majeshi, Jumamosi Aprili 4 Cairo. AFP PHOTO / HO / FADI FARES / EGYPTIAN PRESIDENCY
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Kamati ya juu ya uchaguzi Ayman Abbas, amesema duru ya kwanza itafanyika tarehe 18 na 19 mwezi Oktoba huku duru nyingine ikifanyika tarehe 22 na 23 mwezo Novemba.

Uchaguzi huu ulikuwa umepangwa kufanyika mwezi Machi lakini ukaahirishwa baada ya Mahakama kuamuru kuwa sheria ya uchaguzi ilikuwa kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Misri imekosa wabunge toka mwaka 2012 baada ya Mahakama ilipobadilisha uchaguzi wao baada ya kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani Hosni Mubarak mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.