Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI--USALAMA

Waasi wa Sudan Kusini walinyooshea kidole cha lawama jeshi la serikali

Waasi wa Sudan Kusini wanalituhumu jeshi la Serikali kwa kukiuka mkataba wa kusitisha mapigano, ikiwa ni saa chache zimepita, toka makataa ya kusitisha mapigano yaanze kufanya kazi siku ya Jumamosi.

Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. Lakini, rais wa Sudani Kusini  na mpinzani wake, hawakusiriki katika mazungumzo ya amani, Addis Ababa, Ethiopia.
Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. Lakini, rais wa Sudani Kusini na mpinzani wake, hawakusiriki katika mazungumzo ya amani, Addis Ababa, Ethiopia. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Waasi wamesema wataripoti leo Jumatatu kwa timu ya IGAD ambayo inasimamia mkataba uliotiwa saini.

Msemaji wa waasi wa Riek Machar, Dickson Gatluak amesema kuwa vikosi vya serikali vilishambulia maeneo yao katika mji wa Bor na Panija, na kwamba mashambulizi haya ni wazi yanakiuka makubaliano ya kusitisha mapigano kati yao.

hayo yakijiri mapigano mapya yamezuka katika mji wa Malakal nchini Sudan Kusini, mji mkuu wa jimbo la kuzalisha mafuta la Upper Nile, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Sudan Kaskazini.

Tayari mapigano hayo yamevuruga mkataba uliosainiwa majuzi na rais Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa mashambulizi haya na mvutano wa pande hizi mbili, ni sehemu ya changamoto za utekelezaji wa mkataba huo.

Wachambuzi wa mambo pia wanaona kuwa mashambulizi haya yanatia dosari mkataba uliotiwa saini takriban juma moja lililopita kati ya rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.