Pata taarifa kuu
DRC-ICC-NTAGANDA-SHERIA

DRC: Muasi wa zamani Bosco Ntaganda mbele ya ICC

Kesi ya kiongozi wa zamani wa kivita Bosco Ntaganda, anayetuhumiwa uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ikiwa ni pamoja na ubakaji kwa wanajeshi watoto, itafunguliwa Jumatano wiki hii mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Bosco Ntaganda, Februari mwaka 2015, Hague, Uholanzi.
Bosco Ntaganda, Februari mwaka 2015, Hague, Uholanzi. Reuters
Matangazo ya kibiashara

" Bosco Ntaganda aliajiri mamia ya askari watoto ambao aliwatumia kama watumwa na kuamuru ubakaji uliopangwa kwa wasichana ", amesema leo Jumanne mwendesha mashitaka Fatou Bensouda wakati wa mkutano na vyombo vya habari.

Fatou Bensouda atakua wa kwanza kuzungumza, baada ya kufunguliwa kwa kesi hii saa 03:30 saa za Hague (sawa na 01:30 saa za kimataifa) dhidi ya mtu ambaye anatuhumiwa makosa 13 ya uhalifu wa kivita na makosa matano ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji, uporaji, mashambulizi dhidi ya raia, ubakaji na utumwa wa ngono.

Muasi huyo wa zamani, mwenye umri wa miaka 41 alishirikiana na askari wake kutoka kundi la FPLC, katika ghasia za kikabila na mashambulizi dhidi ya raia katika mji wa Ituri, kaskazini mashariki mwa Congo, mwaka 2002 na 2003.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, FPLC, kundi la wanamgambo wengi wao kutoka kabila la Wahema, walikua wakiwalenga wale wanaonekana kama ni watu kutoka makabila ya walendu, Wabira na Wanande.

Kwa mujibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali, migogoro hii ilisababisha vifo vya zaidi ya watu 60,000.

Hii ni mara ya kwanza katika sheria za kimataifa za uhalifu mtuhumiwa kutakiwa kijubu makosa ya ubakaji na utumwa wa ngono yaliotendwa watoto walikua katika kundi lake.

" Sio kesi ya kundi la kikabila, ni kesi ya mtu ambaye alipitia kwenye mvutano wa kikabila uliokua uliibuka katika mji wa Ituri kwa faida yake binafsi, ili kufikia utawala na mali ", ameongeza Bi Bensouda.

Wakati wa kesi hiyo, upande wa mashtaka unatarajiwa kuwasilisha nyaraka zaidi ya 8,000, ripoti za wataalam, sehemu za video na taarifa mbalimbali. Zaidi ya mashahidi 70 na mashahidi wataalam kadhaa watasikilizwa, Fatou Bensouda amehakikisha.

Bosco Ntaganda, ambaye anajifunza Kiingereza na kupiga piano katika gereza lake katika mjini Hague, amesema hana hatia. Atapewa nafasi ya kujitetea wakati wakili wake, raia wa Canada, Stephane Bourgon, atakua amekamilisha ripoti yake ya ufunguzi.

Ntaganda amezaliwa nchini Rwanda mwaka 1973 katika familia ya Kitutsi ya watoto sita, na baadaye kuhamia nchini Congo miaka ya 1980 katika wilaya ya Masisi jimboni Kivu Kaskazini ambapo amesubiri uasi wa Rwanda wa mwaka 1994 kujiunga na RPF ya Paul Kagame, sanjari na uasi wa Laurent Kabila mwaka 1997 dhidi ya Mobutu Sese Seko miaka miwili baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.