UGANDA-SIASA
Mgombea kwa tiketi ya chama cha FDC kujulikana leo
Zaidi ya wajumbe elfu 1 wa chama cha upinzani nchini Uganda FDC wanapiga kura leo Jumatano kumchagua atakayepeperusha bendera ya chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Kinyanyanyiro ni kati ya kiongozi wa zamani wa chama hicho Dokta Kizza Besigye na Mwenyekiti wa sasa Meja Jenerali Mugisha Muntu.
Besigye na Muntu wamekuwa wakichuana mara kwa mara kupeperusha bendera ya chama hicho na kwa nyakati zote Besigye ameibuka mshindi.
Wajumbe wa chama hicho wanasema wako tayari kumchagua mgombea wao baada ya miezi miwii ya kampeni kumalizika.