Pata taarifa kuu
BURKINA-USALAMA-SIASA

Burkina Faso: mashambulizi ya jeshi dhidi ya RSP yamalizika

Baada ya siku nzima ya wasiwasi Jumanne wiki hii, wanajeshi wa kikosi cha zamani cha ulinzi wa Rais waliokimbilia katika kambi moja ya mji mkuu wa nchi hiyo Ouagadougou hatimaye wamekubali kuweka chini silaha.

Askari polisi akipiga doria karibu na kambi ya NAABA Koom, Septemba 29, 2015.
Askari polisi akipiga doria karibu na kambi ya NAABA Koom, Septemba 29, 2015. REUTERS/Arnaud Brunet
Matangazo ya kibiashara

Jumanne jioni wiki hii jeshi linalounga mkono serikali ya mpito limeendesha mashambulizi katika kambi walikokimbilia wanajeshi wa kikosi cha zamani cha ulinzi wa Rais, baada ya kuzingira kambi hiyo mapema Jumanne asubuhi Septemba 29.

" Kwa sasa tunadhibiti kambi ya NAABA Koom II ", Idara ya mawasiliano ya vikosi vya jeshi la Burkina Faso imesema Jumanne jioni. Mashambulizi ya vikosi vinavyounga mkono serikali ya mpito dhidi wanajeshi wa Kikosi cha zamani cha ulinzi wa Rais yameendeshwa Jumanne alasiri wiki hii. Jeshi limeshambulia kwa makombora kambi walikokimbilia wanajeshi wanaopinga zoezi la kupokonywa silaha. Baada ya jitihada ya kuhimili mashambulizi ya nchi kavu, vikosi vinavyounga mkono serikali ya mpito hatimaye vilitumia uwezo mkubwa kwa kuwadhibiti wanajeshi wa kikosi cha zamani cha ulinzi wa Rais (RSP).

Kwa mujubu wa mkuu wa zamani wanajeshi wa kikosi cha zamani cha ulinzi wa Rais (RSP), jenerali Gilbert Diendéré, mashambulizi hayo yalidumu saa mbili. Mkuu wa majeshi amethibitisha kwamba operesheni katika kambi walikokimbilia wanajeshi wa zamani wa kikosi cha ulinzi wa Rais yalimalizika bila upinzani mkubwa.

Hakuna ripoti yoyote ya operesheni hiyo ambayo imekwishapatikana. " Tunatsubiri kurudi kwa askari wa nchi kavu ili tuweze kujua hasara iliyotokana na mashambulizi hayo ", Idara ya mawasiliano ya jeshi la Burkina Faso imeongeza. Akihojiwa na RFI, Gilbert Diendéré amesema wito wake umeitikiwa na wanajeshi ambao wamekua bado wakipinga kuweka chini silaha. Kabla ya mashambulizi ya vikosi vinavyunga mkono setikali, jenerali Gilbert Diendéré aliwataka wanajeshi wa kikosi cha zamanicha ulinzi wa Rais (RSP) kusalimisha silaha na kuziweka mikononi mwa jeshi la ulinzi wa taifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.