Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Wapinzani wa Kabila wapongeza uamzi wa Katumbi

Kujiuzulu kwa Moïse Katumbi, ambaye alitangaza Jumanne wiki hii kuondoka katika chama cha Rais Joseph Kabila, kumezuia hisia tofauti kwa wanasiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Moïse Katumbi, hapa mjini Lubumbashi mwezi Novemba 2011 katika mkutano na wawakilishi wa MONUSCO, amejiuzulu rasmi katika chama cha PPRD.
Moïse Katumbi, hapa mjini Lubumbashi mwezi Novemba 2011 katika mkutano na wawakilishi wa MONUSCO, amejiuzulu rasmi katika chama cha PPRD. AFP PHOTO / PHIL MOORE
Matangazo ya kibiashara

Upinzani umepongeza uamzi huo ukiutaja kuwa ni wenye “ msimamo na wa busara”, huku msemaji wa serikali akimtahadharisha mshirika wa zamani wa Rais Joseph Kabilakuhusu uwezekano wa kufuatiliwa na vyombo vya sheria.

Kujiuzulu kwa Moïse Katumbi mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga, ni pigo kubwa kwa chama tawala cha PPRD, na kwa serikali kwa jumla, lakini pia ni furah kwa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Moïse Katumbi ameelezea uamzi wake wa kujiuzulu kuwa umesababishwa na uamzi wa baadhi ya viongozi wa kutoheshimu Katiba ya nchi ya Congo.

Upinzani wakaribisha uamzi wa Katumbi

Vyama saba vya kisiasa viliojitenga na vyama vinavyunga mkono utawala wa Kabila vimebaini kwamba vilifanya hivyo ili " kuiokoa katiba ya nchi " na " kutetea kupishana madarakani mwaka 2016 ".

Kwa mujibu wa vyama hivi, rasimu ya sheria juu ya kura ya maoni na ucheleweshaji katika utekelezaji wa kalenda ya uchaguzi ni mifano hai inayonyesha nia ya utawala kusalia madarakani baada ya mwaka 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.