Pata taarifa kuu
EU-BURUNDI-SIASA-VIKWAZO

EU yawachukulia vikwazo maafisa wanne wa Burundi

Umoja wa Ulaya umewachukulia vikwazo maafisa wanne wa jeshi na polisi nchini Burundi walio karibu na Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza.

Un policier patrouille dans les rues de Bujumbura,la capitale, fin juillet.
Un policier patrouille dans les rues de Bujumbura,la capitale, fin juillet. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati wanajeshi na askari polisi ikiwa ni pamoja na baadhi ya maafisa wa jeshi na polisi wakiendelea kutoroka idara hizo.

Umoja wa ulaya umebaini kwamba vikwazo hivyo vimechukuliwa ili kukomesha vitendo viovu dhidi ya binadamu ambavyo vimekua vikiendeshwa na maafisa hao nchini Burundi. Umoja wa Ulaya umezitaka nchi wanachama wa Umoja huo kuzuia mali za maafisa hao pamoja na kupigwa marifiku kuingia barani Ulaya.

Maafisa hao wa jeshi na polisi waliochukuliwa vikwazo ni pamoja na naibu mkuu wa polisi jenerali Godefroid Bizimana, Gervais Ndirakobuca almaarufu Ndakugarika ( afisa muandamizi katika polisi, Joseph Niyonzima (maarufu Kazungu) na jenerali Leonard Ngendakumana mmoja wa maafisa wa jeshi waliendesha jaribio la mapinduzi lililotibuka Mei 13, ambaye alikiri hivi karibuni kuwa wanajeshi wao ndio walikua wakiendesha mashambulizi ya gruneti jijini Bujumbura.

Inasemekana kuwa jenerali Leonard Ngendakumana alikua mmoja wa washirika wa karibu wa Rais Pierre Nkurunziza, na ni mzaliwa wa mkoa wa Ngozi, Kaskazini mwa Burundi, anakozaliwa Pierre Nkurunziza.

Mwanzoni mwa wiki hii naibu mkuu wa kambi ya jeshi ya Muha mjini Bujumbura, meja Emmanuel Ndayikeza pamoja na mkurugenzi wa kitengo cha mawasiliano katika jeshi, kanali Edouard Nshimirimana pamoja na naibu wake, walilitoroka jeshi na kwa sasa hawajulikani waliko. Taarifa hii imethibitishwa na msemaji wa jeshi la Burundi, kanali Gaspard Baratuza, akibaini kwamba maafisa hao wa jeshi wanatafutwa kwa udi na uvumba. Duru za kijeshi zinabaini kwamba kanali Edouard Nshimirimana ametoroka na vifaa mbalimbali vya mawasiliano ya jeshi, na ndiye aliyekuwa akihusika na masuala yote ya mawasiliano katika jeshi la Burundi.

Hayo yanajiri wakati hali ya taharuki imeendelea kutanda nchini Burundi, hasa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.