Pata taarifa kuu
BURUNDI-RWANDA-DIPLOMASIA

Mshauri mkuu wa ubalozi wa Rwanda afukuzwa Burundi

Afisa mmoja wa Ubalozi wa Rwanda mjini Bujumbura amefukuzwa kuondoka nchini Burundi na kurejea nchini mwake kwa tuhuma za kuingilia masuala ya ndani ya nchi ya Burundi kufuatia mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (kulia).
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza (kulia). AFP PHOTO/JOSE CENDON
Matangazo ya kibiashara

Désiré Nyahuririra ambaye ni mshauri wa Balozi wa Rwanda nchini Burundi amefukuzwa nchini Burundi na kulazimika kuondoka ndani ya saa chache zijazo kulingana na Ibara ya 9 ya Mkataba wa Vienna kuhusu Mahusiano ya kidiplomasia, imetangazwa na serikali ya Burundi bila kutoa maelezo zaidi.

Kwa Upande wa serikali ya Rwanda, Wizara ya Mombo ya Nje imesema kuwa haina taarifa yoyote ya kufukuzwa kwa mwanadiplomasia wake, na kuamini kuwa huenda jambo hilo likawa kweli kwa vile ukaidi na uzembe wa Serikali ya Burundi vinaelekea kulipelekea taifa hilo katika dimbwi la machafuko, amesema afisa mmoja wa serikali ya Rwanda.

Désiré Nyahuririra amekuwa mtu muhimu katika kuhakikisha mahusiano ya Rwanda na Bujumbura yanaimarika kwa njia ya maridhiano baina ya chama cha CNDD-FDD na Rwanda, hasa kupitia kwa Jenerali wa Burundi Adolphe Nshimirimana aliyeuawa mwezi Agosti uliopita.

Kufukuzwa kwa Désiré Nyahuririra ni hatua nyingine katika mdororo wa Mahusiano baina ya Rwanda na Burundi ambapo Rwanda inanyooshewa kidole na serikali ya Burundi kuwapa mafunzo ya kijeshi waasi wa Burundi, huku Burundi nayo ikidaiwa kuwahifadhi waasi wa kihutu wa Rwanda wa FDLR.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.