Pata taarifa kuu
ICC-LRA-SHERIA-HAKI

Ofisi ya Mashtaka ya ICC yamuongezea mashtaka Dominic Ongwen

Ofisi ya kiongozi wa Mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya ICC inasema imemwongezea mashtaka kiongozi wa juu wa kundi la LRA Dominic Ongwen.

Dominic Ongwen, mmoja wa viongozi wakuu wa kundi la waasi wa Uganda wa LRA, wakati wa kesi yake ya kwanza mbele ya Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC) Jumatatu, Januari 26, 2015.
Dominic Ongwen, mmoja wa viongozi wakuu wa kundi la waasi wa Uganda wa LRA, wakati wa kesi yake ya kwanza mbele ya Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC) Jumatatu, Januari 26, 2015. REUTERS/Peter Dejong
Matangazo ya kibiashara

Ongwen ambaye alikuwa ameshtumiwa kutekeleza makosa saba sasa amefunguliwa mashtaka mengine 60.

ICC inaendeleza uchunguzi wake dhidi ya Ongwen ambaye kundi lake liliwauawa na kuwateka watu Kaskazini mwa Uganda, nchini Jamhur ya Kidemokrasia ya congo, nchini Sudan na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kesi dhidi ya Ogwen inatarajiwa kuanza tarehe 21 mwezi Januari.

Kiongozi Mkuu wa LRA Joseph Kony anaendelea kutafutwa na wanajeshi wa Uganda kwa usaidizi wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.