Pata taarifa kuu
BURUNDI-EALA-USHIRIKIANO

Burundi yalitaka Bunge la EALA kuwaagiza wabunge wake nyumbani

Spika wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki EALA Dan Kidega amesema amepokea barua kutoka Burundi, ikimtaka kuwaagiza wabunge wa nchi hiyo kurudi nyumbani.

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. RFI / SR
Matangazo ya kibiashara

Agizo hilo kutoka Bunge la Burundi kutaka wabunge wake wanne wanaowakilisha nchi hiyo kwenye Bunge hili linakuja wakati huu vikao vya EALA vikiendelea jijini Kigali nchini Rwanda kwa siku ya pili leo Jumanne.

Vikao hivyo vitaendelea jijini Kigali kwa muda wa wiki zijazo na hatua hiyo ya Burundi kurudi nyumbani inaelezwa na wachambuzi wa siasa kuwa huenda ni kwa sababu ya tofauti za kisiasa kati ya Rais Paul Kagame na Pierre Nkurunziza.

Rais Kagame ameendelea kumshutumu Rais Nkurunziza kutokana na machafuko yanayoendelea katika nchi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.