Pata taarifa kuu
TUNISIA-SHAMBULIZI-USALAMA

Tunisia: IS yakiri kuhusika na mashambulizi dhidi ya kikosi cha usalama wa rais

Kundi la Islamic State (IS), katika taarifa yake iliyorushwa hewani Jumatano hii kwenye mitandao ya makundi ya kijihadi, limekiri kuhusika na shambulizi dhidi ya basi la kikosi cha usalama wa usalam wa rais nchini Tunisia.

Wachunguzi wa polisi ya sayansi watoa dalili kwenye mabaki ya basi la usalama wa rais lililolengwa na shambulizi la bomu katikati mwa mji wa Tunis, Novemba 25, 2015.
Wachunguzi wa polisi ya sayansi watoa dalili kwenye mabaki ya basi la usalama wa rais lililolengwa na shambulizi la bomu katikati mwa mji wa Tunis, Novemba 25, 2015.
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii inakuja siku moja baada ya shambulizi hilo lililogharimu maisha ya watu 12 katikati mwa mji mkuu wa Tunisia, Tunis.

Muhusika wa mashambulizi ni raia wa Tunisia aliyetambuliwa kama "Abu Abdallah al-Tounissi". Akivalia mkanda wa kulipuka, mshambuliaji huyo aliingia katika basi, na akajilipua," kulingana na taarifa hiyo iliyotolewa na kundi la Islamic State.

Kundi hilo pia limetoa picha ya mtu huyo, akiwa amevaa mavazi meupe na amevaa mkanda wa kulipuka, huku akinyoosha kidole juu, kichwa na uso vikifunikwa skafu.

Kundi la IS limethibitisha kuwa watu 20 wameuawa katika shambulizi hilo, lakini kwa mujibu wa ripoti rasmi, maafisa 12 wa usalama wa rais waliuawa Jumanne wiki hii katika shambulizi hilo. Mwili wa kumi na tatu, ambao viongozi wa Tunisia wanasema huenda ni wa muhusika wa shambulizi hilo, umekutwa katika eneo la tukio na umeanza kufanyiwa uchunguzi ili uweze kutambuliwa, wizara ya mambo ya ndani imebaini.

Shambulizi hilo lilitekelezwa kwa msaada wa kilo kumi za vilipuzi , wizara ya mambo ya ndani imeongeza, huku ikieleza kuwa kifaa kiliotumiwa kilikua Semtex, moja ya vilipuzi vyenye nguvu zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.