Pata taarifa kuu
AMNESTY INTERNATIONAL-DRC-HAKI-SIASA

Amnesty International yainyooshea kidole seriklai ya DRC

Shirika la kimataifa linalotetea haki za binadamu la Amnesty International limeikosoa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kutumia vibaya mamlaka ya kisheria nchini humo katika kuminya uhuru wa watu ambao wanapinga jaribio la rais anayemaliza muhula wake mwaka ujao nchini humo wa kutaka kuwania muhula wa tatu.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila (kulia) akiwasili kwenye uwanja wa Mavivi, wakati wazira yake katika mji wa Beni, Oktoba 29 mwaka 2014.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila (kulia) akiwasili kwenye uwanja wa Mavivi, wakati wazira yake katika mji wa Beni, Oktoba 29 mwaka 2014. AFP PHOTO / ALAIN WANDIMOYI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapioshwa na shirika la Amnesty International, ni kuwa vyombo vya sheria nchini Jamhuri ya Kidemokrasi aya Congo vimedhibitiwa na mamlaka ya nchi hiyo, kwa lengo la kuwanyamazisha wanasiasa au wanaharakati wanaodhihirisha msimamo wao wa kupinga harakati za kuurefusha muda wa utawala wa rais Joseph Kabila.

Wakati wa maandamano dhidi ya serikali ya Joseph Kabila, polisi ikitumia mbinu za kuwakamata waandamanaji, Januari 19, 2015 mjini Kinshasa.
Wakati wa maandamano dhidi ya serikali ya Joseph Kabila, polisi ikitumia mbinu za kuwakamata waandamanaji, Januari 19, 2015 mjini Kinshasa. AFP/Papy Mulongo

Upande wa chama tawala cha PPRD na hali kadhalika katika vyama vinavyomuunga mkono rais Joseph Kabila, wanaona kuwa hakuna ukweli wowote katika ripoti hii ya Amnesty International.

Licha ya kuwa hakuna taarifa zozote kutoka kwa rais Kabila za kutaka kuwania muhula wa tatu, upinzani nchini DRC, hata hivyo, umekuwa ukilalamikia kuwepo na mbinu za vyama vinavyomuunga mkono rais huyo, za kumuandalia mwanya wa kuwania muhula huo.

Ripoti hii mpya ya Amnisty International pia imesema wengi baadhi ya wanasiasa waliojitokeza kupinga mabadiliko ya katiba katika harakati za kumruhusu rais Joseph Kabila kuwania muhula wa tatu, miongoni mwao Jean Louis Ernest Kyaviro, na wanaharakati wengine bado wanaendelea kushikiliwa na vyombo vya usalama katika nchi hiyo, huku wengine wakinyimwa haki zao za kimsingi za kibainadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.