Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-UCHAGUZI-SIASA

Burkina Faso: matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa kutangazwa Jumatatu

Mamia kwa maefu ya raia wa Burkina Faso wamepiga kura Jumapili hii Novemba 29 katika hali ya utulivu kwa kumchagua rais wao mpya, "uchaguzi wa kihistoria" unaofanyika mwaka mmoja baada ya Blaise Compaoré kung'atuliwa madarakani.

Zoezi la kuhesabu kura chini ya uangalizi wa waangalizi wa uchaguzi wa rais na wabunge, katika kituo cha kupigia kura cha Ouagadougou, Novemba 29, 2015.
Zoezi la kuhesabu kura chini ya uangalizi wa waangalizi wa uchaguzi wa rais na wabunge, katika kituo cha kupigia kura cha Ouagadougou, Novemba 29, 2015. © REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Mamia kwa maefu ya raia wa Burkina Faso wamepiga kura Jumapili hii Novemba 29 katika hali ya utulivu kwa kumchagua rais wao mpya, "uchaguzi wa kihistoria" unaofanyika mwaka mmoja baada ya Blaise Compaoré kung'atuliwa madarakani.

Blaise Compaoré aliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi, na kuiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 27.

Watu milioni 5.5 waliojiandikisha kupiga kura wameitwa kushiriki katika uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa wabunge, kabla ya kubadili ukurasa wa utawala wa mpito uliowekwa baada ya maandamano makubwa yaliomng'oa madarakani Blaise Compaoré mwezi Oktoba mwaka 2014, wakati ambapo alikua akijaribukuifanyia marekebisho Katiba ili aweze kuwania muhula mwengine.

"Mara baada ya bosi mkubwa kutokuwepo, sasa uchaguzi unafanyika kwa uhuru zaidi na kidemokrasia", Ousmane François Ouedraogo, mwenye umri wa miaka 65, ambaye ni mmoja wa wapiga kura amepongeza, akiwafananisha na wakati wa utawala wa "Blaise Compaoré", aliye uhamishoni katika nchi jirani ya Côte d'Ivoire.

Awali uchaguzi huu ulipangwa kufanyika Oktoba 11, lakini uliahirishwa kutokana na mapinduzi ya kijeshi Septemba 17, mapinduzi ambayo yaliongozwa na mtu wa karibu wa Blaise Compaoré, jenerali Gilbert Diendéré na kushindwa utokana na msimamo wa raia na majeshi tiifu kwa Rais Michel Kafando.

Matarajio ni mengi katika nchi hii maskini ya Afrika Magharibi yenye wakazi walio chini ya milioni 20, ambayo inataka kuona katika uchaguzi huu mwanzo wa kipindi chenye misingi ya kidemokrasia.

Wagombea kumi na wanne wakiwemo wanawake wawili wamekuwa wanawania kiti cha urais kwa kipindi cha miaka mitano ambacho kinaongezwa mara moja.

Roch Marc Christian Kaboré na Zéphirin Diabré, mawaziri wa zamani wawili walioingia katika upinzani kabla ya Blaise Compaoré kun'gatuliwa madarakani, wanapewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.