Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA

Rais Zuma akubali kulipa sehemu ya fedha zilizotumika kufanya ukarabati wa makazi yake

Rais wa Afrika Kusini, Jackob Zuma amependekeza kwa mahakama ya katiba nchini humo kumuagiza waziri wa fedha na mkaguzi mkuu wa Serikali kufanya tathmini na kuamua ni kiasi gani anachopaswa kulipa baada ya kufanyika ukarabati wa makazi yake binafsi mjini Nkandla.

Jacob Zuma, rais wa Afrika kusini
Jacob Zuma, rais wa Afrika kusini Reuters/Sumaya Hisham
Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa yake rais Jackob Zuma, ameuita uamuzi wake kuwa ni zaidi na utashi wa kisiasa na kwamba hataki kuingilia mamlaka yoyote katika kutekeleza jukumu lake.

Rais Jackob Zuma aliwasilisha mapendekezo hayol katika mahakama ya juu ya nchi hiyo siku ya Jumanne akitarajia uamuzi kutolewa hivi karibuni.

Uamuzi wake ameufanya ikiwa ni wiki moja tu imesalia kabla ya mahakama ya katiba nchini humo kaunza kusikiliza kesi dhidi yake, hatua ambayo rais Zuma anasema inalenga kuondoa utata uliokuwepo kuhusu matumizi ya fedha za umma kwaajili ya ukarabati uliofanywa nyumbani kwake.

Julius Malema, kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters
Julius Malema, kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters AFP PHOTO / MUJAHID SAFODIEN

Chama cha upinzani nchini humo cha Economic Freedom Fighter kiliamua kupeleka suala hilo katika mahakama ya katiba ili itoea uamuzi, baada ya kamati ya bunge kuidhinisha ripoti ya waziri wa sheria iliyomsafisha Zuma dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

Rais Zuma amesema yuko tayari kulipoa kiasi cha fedha anachodaiwa, na kwamba safari hii waziri wa fedha na mkaguzi mkuu wa Serikali ndio wanaopaswa kuamua ni kiwango gani anatakiwa kukirejesha.

Hata hivyo rais Zuma amesisitiza kile anachokiamini kuhusu ripoti ya mkuu wa jopo lililoundwa kuchunguza matumizi ya fedha za uma kufanya ukarabati wa makazi yake, ambapo ripoti hiyo ya mwaka 2014 ilipendekeza kiongozi huyo kurejesha kiasi hicho cha fedha.

Licha ya uamuzi huu wa rais Zuma, chama cha upinzani cha Democratic Alliance na kile cha Julius Malema EFF, vimesema vitaendelea mbele na kesi yao waliyoifungua kwenye mahakama ya katiba kudai haki.

Zuma anadaiwa kutumia kiasi cha dola za Marekani milioni 24 kufanya ukarabati wa makazi yake binafsi, fedha ambazo upinzani unadai hazikupaswa kutumiwa na kiongozi huyo kwakuwa zilikuwa ni fedha za uma kwaajili ya shughuli za maendeleo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.