Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI

Uongozi wa waasi wa Sudan Kusini waunga mkono mapendekezo mapya ya wakuu wa IGAD

Uongozi wa waasi wa Sudan Kusini, juma hili umekaribisha kwa mikono miwili mapendekezo ya viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano na Maendeleo IGAD, ambao wanataka kuahirishwa kwa mpango wa ugawaji wa majimbo mengine 28 yaliyotangazwa na Serikali.

Mpatanishi mkuu wa kundi la waasi wa Sudan Kusini, Taban Deng Gai
Mpatanishi mkuu wa kundi la waasi wa Sudan Kusini, Taban Deng Gai REUTERS/Goran
Matangazo ya kibiashara

Waasi wanaoongozwa na Riek Machar wanataka kwanza kuundwa kwa Serikali ya umoja wa kitaifa kabla ya kuundwa kwa majimbo hayo 28, ambayo inasema uundwaji wake ulienda kinyume na makubaliano.

SPLM-IO inasema kuwa uamuzi wa kisiasa uliochukuliwa na rais Salva Kiir nje ya mkataba wa amani walioutia saini, unaonekana na kundi hilo kama mapendekezo ambayo haya msingi wa kisheria a nikinyume na makubaliano waliyotia saini mwezi August mwaka jana.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya Serikali ya Juba, yenyewe inasema inakubaliana kwa asilimi mia moja na mapendekezo ya wakuu wa IGAD lakini wao wanajikita zaidi katika pendekezo lao la uundwaji wa Serikali ya kitaifa.

Jumuiya ya IGAD ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari siku ya jumapili, ikizitaka pande zote zinazohusika kwenye mzozo wa Sudan Kusini, kutekeleza makubaliano waliyotia saini mwezi August mwaka jana na kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa bila kubadili katiba iliyopo sasa.

IGAD kwenye taarifa yake, imemtaka rais Salva Kiir kuahirisha mpango wake wa awali alioutangaza wa kuunda majimbo mapya 28 aliyoyatangaza October 2 siku chache baada ya kutia saini makubalino ya amani, na kwamba uamuzi wake unaenda kinyume na maelekezo ya IGAD na mkataba wenyewe wa amani.

IGAD yenyewe inasema inatambua majimbo 10 pekee ambayo yalikuwepo awali chini ya katiba inayosimamia nchi hiyo kwa sasa.

Taarifa ya IGAD pia imewataka viongozi wa pande zote mbili kuunda kamati maalumu ya kupitia mipaka ya nchi, kamati ambayo itakuwa na jukumu la kupitia upya mapendekezo ya rais kuhusu uundwaji wa majimbo mengine mapya na kwamba ikiwa hawatakubaliana, basi wasalie na majimbo 10 yaliyokuwepo awali.

Msemaji wa kundi hilo, James Gatdet Dak, amesema kwa upande wo wanakaribisha mapendekezo ya wakuu wa IGAD na kwamba wao toka awali walikuwa tayari kutekeleza mkataba wa amani walioutia saini, na wanatambua majimbo 10 yaliyokuwepo awali.

James Gatdet Dak, anasema kama Serikali inataka kuunda majimbo mengine, basi kwanza watekeleze mkataba wa amani kwa kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa na kisha ndio uanze mchakato wa mazungumzo ya uundaji wa majimbo mengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.