Pata taarifa kuu
LIBYA-UN

Wabunge 10 wa bunge linaloungwa mkono na makundi ya kiislamu nchini LIbya, wafutwa kazi

Bunge la Libya linaloungwa mkono na makundi ya kiislamu, juma hili limewafuta kazi wabunge wake 10 ambao walitia saini mkataba wa amani uliokuwa unasimamiwa na Umoja wa Ulaya ili kuwezesha kuundwa kwa Serikali ya umoja wa kitaifa.

Wajumbe wa Libya wakitia saini mkataba wa amani hivi karibuni
Wajumbe wa Libya wakitia saini mkataba wa amani hivi karibuni REUTERS/Zoubeir Souissi
Matangazo ya kibiashara

Naibu wa kwanza wa spika wa bunge hilo, Awad Mohammed Abdul-Sadiq, amewaambia waandishi wa habari kuwa, wamewamua kuwafuta kazi wabunge ambao walitia saini makubaliano yamwezi December mwaka jana nchini Morocco.

Mohammed ameongeza kuwa uamuzi wa kuwafuta kazi wabunge hao ulifikiwa baada ya kikao kilichofanyika mwishoni mwa juma, na kuongeza kuwa wabunge hao hawakuwa na idhini ya kutia saini makubaliano hayo na hivyo walikiuka katika ya mwaka 2011.

REUTERS/Mandel Ngan/Pool

Kwa mujibu wa maeleo yake, miongoni mwa wabunge waliofutwa kazi ni pamoja na makamu wa rais wa bunge hilo, Saleh el-Makhzoum.

Nchi ya Libya ina mabunge mawili yanayovutana huku bunge moja tu la Tripoli ndio linalotambuliwa na jumuiya ya kimataifa, ambapo mabunge hayo yamekuwa yakifanya kazi toka mwaka 2014.

Kati kati ya mwezi December mwaka jana, ni robo tatu tu ya wabunge wa mabunge yote mawili ndio waliotia saini mkataba wa amani unaofanya pande hizo kuunda Serikali ya umoja wa kitaiafa.

Serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa inaongozwa na mfanyabiashara Fayez al-Sarraji ambapo ameunda baraza la mawaziri 32.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.