Pata taarifa kuu
A.KUSINI-AJALI

Juhudi za uokozi zaendelea katika mgodi wa dhahabu A. Kusini

Timu za uokozi zinanedelea na juhudi za kuwaokowa wachimba migodi wakiwa hai ambao wamekwama katika vifusi vya udongo leo ikiwa ni siku ya tatu. Abednego Magongo wa shirika la wafanyakazi wa mgodini AMCU amesema wanafanya kila jitihada kuwaokowa watu hao wakiwa hai.

wafanyakazi wa mgodini nchini Afrika Kusini wakiwa ndani ya bus
wafanyakazi wa mgodini nchini Afrika Kusini wakiwa ndani ya bus REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Mgodi huo uliporomoka tangu Ijumaa wakati nguzo mbili zilipovunjika na kusababisha mporomoko wa mgodi ho wa dhahabu wa Lily de Vantage Goldfields katika jimbo la Mpumalanga kaskazini mashariki, wafanyakazi hao watatu walikuwa chini ya mgodi wakati wa ajali hiyo.

Jumla wafanyakazi 87 waliokuwa wakifanyakazi kwenye mdogo ho waliokolewa haraka. Waokozi walifaulu kufaham uwepo wa watu hao chini ya mgodi kupitia mitambo ya mawasiliano ya redio.

Mkurugenzi wa kiwanda hicho cha mgodi wa dhahabu Mike Begg alizungumzia kupia chombo cha habari nchini Afrika Kusini cha Eye Witness News kwamba walipata kiashiria cha uwepo wa watu chini ya mgodi huo baada ya mazungumzo kupitia mawasiliano ya redio na hivyo wamezidisha juhudi na kasi katika maeneo hayo kuhakikisha watu hao wanaokolewa wakiwa hai.

Katika operesheni za ukozi, tani kadhaa za udongo na mawe viliondolewa, huku familia za watu waliopotea zikiandaa ibada ya misaa ya kuwaombea mwishoni mwa juma lililopita.

Afrika Kusini, yenye migodo mingi, imekumbwa na ajali mara kadhaa katika miaka ya hivi karibuni.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.