Pata taarifa kuu
COMORO-UCHAGUZI

Mjadala waibuka nchini Comoro kuhusu kisiwa cha Mayotte

Februari 8 mwaka 1976 wananchi wa kisiwa cha Mayote walipiga kura ya maoni ya kuamuwa kwa asilimia 99 kisiwa hicho kubaki upande wa Ufaransa. Na kimebaki kisiwa pekee cha Comoro ambacho hakichaomba uhuru wake mwaka 1975. Lakini miaka 40 baadae mjadala umeibuka tena nchini Comoro wakati huu wa uchaguzi mkuu wa rais kuhusu kisiwa hicho cha Mayotte.

Matangazo ya kibiashara

Kumekuwa na mjadala mkuwa kila unapofikia uchaguzi nchini Comoro kuhusu kisiwa cha Mayotte ambacho kipo chini ya serikali ya Ufaransa. Wagombea zaidi ya 20 katika uchaguzi mkuu wa rais nchini Comoro wamekuwa wakitofautiana na kuhusu swala hili na mbinu za kukirejesha upande wa Comoro.

Baadhi wanapendekezo uswepo wa mazungunzo kati ya pande tatu, wengine wanaona kwamba maendelea ya kicuhumi ya visiwa vitatu yanaweza kutatua hali hiyo. Kundi doko linapendekeza kukatisha kabisa uhusiano wa kidiplomasia na Ufaransa ambayo haipashzi kuchukuliwa kama nchi rafiki kwani imekuwa ikikalia kinyume cha sheria kisiwa cha Mayotte ambacho ni cha Comoro kama ilivyoelezwa na Umoja w Mataifa.
Kila mikutano ya hadhara, wagombea wote wamekuwa wakigusia swala hili la kisiwa cha Mayotte, licha kwamba wananchi wengi wa Comoro wanaguswa zaidi na maswala ya Afya, Elimu, Nishati, swala hilo la Mayotte limebaki kuwa swala ambalo linaweza kujadiliwa na serikali yoyote.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.