Pata taarifa kuu
Marekani-Umeme

Rais Obama aidhinisha sheria ya uwekezaji umeme barani Afrika

Rais wa Marekani Barack Obama ameidhinisha jana sheria iliopasishwa na bunge juma lililopita inayo lenga kutowa nafasi kwa sketa binafsi kuwekeza barani Afrika katika sekta ya nishati ili kuwapatishia umeme watu zaidi ya milioni hamsini wa ziada. Sheria hiyo iliidhinishwa bila pengamizi lolote na baraza la wawakilishi baada ya baraza la seneti.

Rais wa Marekani Barack Obama,  picha iliopigwa Februari 5, 2016 katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu ya White House.
Rais wa Marekani Barack Obama, picha iliopigwa Februari 5, 2016 katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu ya White House. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Sheria hiyo haitowi fedha upya, lakini inahitaji utawala wa Marekani kuratibu mkakati ili kuhamasisha sekta binafsi na mashirika ya kimataifa kuwekeza katika umeme barani Afrika na kusini mwa Sahara, ambapo 70% ya wakazi wa eneo hilo hawana umeme, ikiwa ni sawa na watu milioni 600, kwa mujibu wa Ed Royce mbunge wa chama cha Republican

Upande wake Seneta Chris Coons wa chama cha Demokrate amesema, upatikanaji wa nishati ya kuaminika itawarahisishia watoto kufanya kazi zao za shule nyumbani wakiwa katika mazingira mazuri, hospitali zitatumia mashine ili kutambua ugonjwa, na jokofu zitafanya kazi ili kuzuzi chakula kutooaza.

Sheria hiyo iliodhinishwa ina lengo la kuboresha mpango wa Umeme barani Afrika, ambayo Marekani huchangia dola bilioni saba, ambazo rais Obama obama aliahidi wakati was ziara yake nchini Kenya mwezi Julai mwaka jana.

Mwenyekiti ya kamati ya mambo ya nje Seneta Bob Corker amesema Sheria hiyo mpya inataka mashirika mbalimbali ya serikali ya Marekani ya misaada ya maendeleo kutia kipaumbele katika mikopo na dhamana kwa ajili ya miradi ya binafsi ya umeme katika bara la Afrika.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.