Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SIASA

Chama cha ANC kinataraji majibu ya tatizo la ajira kupitia hotuba ya rais Zuma

Chama tawala nchini Afrika Kusini, cha African National Congress, ANC, kinasema kuwa hotuba ya rais kwa taifa ya mwaka 2016 ni lazima itoe jibu na matumaini kwa vijana ambao hawana ajira na wale ambao wanaishi kwenye hali ya umasikini.

Rais Jacob Zuma na Makam wake Cyrill Ramafosa januari 9
Rais Jacob Zuma na Makam wake Cyrill Ramafosa januari 9 REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Rais Jackob Zuma baadae hii leo anatarajiwa kulihutubia bunge katika hotuba yake ya mwaka kwa taifa, wakati huu taifa hilo likikabiliwa na changamoto za kiuchumi pamoja na hali ya ukame iliyokumba maeneo mengi ya nchi.

Katibu mkuu wa ANC amesema anatarajia hotuba ya rais itoe majibu ya changamoto zinazoikabili nchi hiyo, ikiwemo umasikini, hali ngumu ya uchumi na demokrasia ambayo katika siku za hivi karibuni imekosolewa.

Wananchi wengi na hasa waliopiga kura kwenye uchaguzi uliopita, wanataka kusikia rais atajibu vipi hoja za vyama vya upinzani nchini humo ambavyo vinazidi kukosoa utawala wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.