Pata taarifa kuu
UGANDA-LRA

Kiongozi wa LRA aliekamatwa ni Okot Obed

Polisi nchini Jamhuri ya Afrika ya kati imesema imemkamata mmoja kati ya viongozi wa kijeshi wa kundi la Lords Resistance Army LRA linalo tuhumiwa kutekeleza makosa mbalimbali ikiwemo mauaji ya kivita ambae ni kamanda Okot Odek.

Waasi wa LRA mwezi Septemba mwaka 2006 katika mpaka kati ya Sudan na DRC.
Waasi wa LRA mwezi Septemba mwaka 2006 katika mpaka kati ya Sudan na DRC. AFP PHOTO/STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Duru kutoka nchini Jamhuri ya Afrika ya kati zinaeleza kwamba kiongozi huyo alikamatwa na kukabidhiwa kikosi cha Marekani kinachoshirikiana na Uganda katika kuwasaka viongozi wa kundi hilo la LRA linaloongozwa na Joseph Kony.

Kamanda huyo Okot Odek amekamatwa akiwa katika mji wa Obo iliopo mashariki mwa jamhuri ya Afrika ya kati ambako wanajeshi wa Uganda na Marekani wamepiga kambi kuwasaka viongozi wa kundi hilo.

kundi moja lililojitenga kutoka kundi la waasi wa Seleka lilitangaza hapo jana kuwa limemkamta kamanda mmoja aliejitambulisha kwa jina la kijeshi kuwa ni Kamanda Sam, na kumkabidhi kwa vikosi vya Marekani

lakini baadae mwenyewe pamoja na baadhi ya wapiganaji wake waliojisalimisha walijitambulisha kwa jina la Okot Odek, na baadae walikabidhiwa kwa kikosi cha Marekani na Uganda

kwa Mujibu wa shirika moja la Marekani la Invisbile Children linalopiga vita vitendo vya ukatili vinavyotekelezwa na kundi hilo limesema Oket angeliweza kujisamilisha na sio kukamatwa.

kupitia mtandao wake wa internet shirika hilo linasema kuwa oket anawezakuwa alijisalmisha baada ya kuwa na hofu huenda Joseph Kony alitowa amri ya kuuawa kwake, jambo ambalo hutekelezwa mara kadhaa na joseph Kony kwa viongozi wake wa kijeshi wasiokuwa na faida naye tena.

Shirika hilo limesema ujumbe wa Odek unaotowa wito kwa wapiganaji wa LRA walipo nchini jamhuri ya Afrika ya kati na jamhuri kidemokrasia ya congo upo tayari kupeperushwa kupitia radio za maeneo hayo.

hartuwa hii ya kukamatwa kwa kiongozi huyo inakuja ikiwa ni siku kadhaa baada ya kutokea kwa mashambulizi ya kundi la LRA katika majimbo ya Zemio, Bakouma na Bangassou mashariki na kaskazini mwa jamhuri ya Afrika ya kati ambapo watu kadhaa walipoteza maisha huku wengine wakitekwa.

Kundi la wapiganaji zamani la Seleka lilitangaza mwezi Januari mwaka jana kumtia nguvuni Dominc Ongwen kiongozi wa zamani wa kivita wa LRA ambae kwa sasa yupo mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC na ambae kesi yake ilisikilizwa januari 21 na anatuhumiwa makosa 70 ya mauaji ya kivita na mauaji dhidi ya ubinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.