Pata taarifa kuu
MISRI-WANAHABARI

Jengo la waandishi wa habari lavamiwa na polisi

Polisi wa Misri walivamia Jumapili usiku makao makuu ya chama cha waandishi wa habari mjini Cairo, nchini Misri.

Aprili 28, 2016, waandishi wa habari wameandamana mbele ya makao makuu ya chama cha wanahabari dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri.
Aprili 28, 2016, waandishi wa habari wameandamana mbele ya makao makuu ya chama cha wanahabari dhidi ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Misri. REUTERS/Mohamed Abd El Ghan
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya usalama viliwakama waandishi wa habari wawili ambao walikua walikimbilia katika jengo hilo baada ya maandamano ya Aprili 25, dhidi ya uamuzi wa serikali ya Misri kuikabidhi Saudi Arabia visiwa viwili viliyokua chini ya milki yake.

Kamwe katika historia yake ya muda mrefu, makao makuu ya chama cha waandishi wa habari nchini Misri 'yalikua hayajavamia na polisi.

Chama hiki cha wanahabari nchini Msri kiliadhimisha hivi karibuni miaka 75 ya uhai wake na kilikua kinachukuliwa kama kina kinga ya kutoingiliwa kikazi au kuvamiwa na tawala mbalimbali zilizotangulia nchini humo

Uvamizi huo wa polisi ulitekelezwa Jumapili wakati ilishehrekewa Siku ya Kazi duniani na kuibua hali ya sintofahamu siku ya Jumatatu, hata kama ilikua siku ya mapumziko. Kiongozi wa chama cha wanahabari ameomba Waziri wa Mambo ya Ndani achishwe kazi wakati ambapo waandishi wa habari kadhaa walisitisha likizo zao kwa kuja kushirikiana na wenzao kuandaa maandamano.

Kutokana na maandamano kuongezeka na tuhuma mbalimbali kwenye vyombo vya habari tofauti, Wizara ya Mambo ya Ndani imeeleza kitendo chake kutokana na kwamba kulikua na kibali cha kukamatwa kilichotolewa na Ofisi ya mahitaka. Madai hayo yalitupiliwa mbali na waandishi wa habari.

Chama cha wanahabari chafungua mashitaka

Yehia Qalash, kiongozi wa chama cha waandishi wa habari ameamua kutoa kauli kali dhidi ya polisi ambayo inaendelea kuzingira makao makuu ya chama hicho. Watu pekee ambao wana kadi za vyombo vya habari wanaweza kuelekea kwenye makao makuu ya chama cha wanahabari. Katika mkutano na wanahabari, Qalash ameishtumu Wizara ya Mambo Ndani kufanya uhalifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.