Pata taarifa kuu
MISRI-EGYPTAIR

Ajali ya ndege ya EgyptAir: Mabaki bado hayajapatikana

Ndege ya shirika la ndege la EgyptAir liliyokua ikifanya safari kutoka mjini Paris kwendakatika mji wa Cairo ilipata ajali Alhamisi Mei 19 katika pwani ya kisiwa cha Ugiriki ikiwa na watu 66.

Ndege ya jeshi la anga la Misri ikishiriki katika zoezi la kutafuta ndege ya EgyptAir iliyotoewka juu ya bahari ya Mediterranean Mei 19, 2016 (video ya jeshi).
Ndege ya jeshi la anga la Misri ikishiriki katika zoezi la kutafuta ndege ya EgyptAir iliyotoewka juu ya bahari ya Mediterranean Mei 19, 2016 (video ya jeshi). Egyptian Military/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Raia 30 Msri na 15 kutoka Ufaransa ni miongoni mwa abirtia waliopoteza maisha katika ajali hiyo. uchunguzi unaendelea ili kujua sababu za ajali na kujua wapi ilipoangukia.

Kinachofahamika kwa ajali ndege hiyo :

► Ndege hiyo ya EgyptAir iliondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Roissy-Charles de Gaulle saa 5:09 usiku (saa za Paris na Cairo) na watu 66 (Wamisri 30 na Wafaransa 15). Ndege hii yenye chapa MS804 ilipoteza mawasiliano na mitambo ya rada wakati ilipoingia katika eneo la anga la Misri juu ya bahari ya Mediterranean.

► Mabaki ya Airbus A320 bado hayajapatikana. Naibu kiongozi wa shirika la ndege la Egyptair Ahmed Adel, amlirejelea Alhamisi Mei 19 kauli aliyoitoa kwenye runinga ya CNN akitangaza kugunduliwa kwa mabaki ya ndege hiyo MS804. Mapema jioni, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa Anga nchini Ugiriki alikanusha tangazo lililotolewa na mkurugenzi washirika hilo la ndege la ya Misri.

► Taasisi ya Uchunguzi na Tathmini (BEA) na kampuni ya Airbus zimewametuma wataalamu. Wapelelezi watatu kutoka Taasisi ya Uchunguzi na Tathmini wakiongozana na mshauri wa kiufundi wa Airbus wataungana serikali ya Cairo kwa kuendesha uchunguzi. Wachunguzi wataondoka mjini Paris jioni na wanatarajiwa kuwasili mjini Cairo usiku.

► Mapema Alhamisi hii mchana Waziri wa Misri mwenye dhamana ya usafiri wa anga alisema kuwa kuna uwezekano kuwa ndege hiyo imekumbwa na shambulio la kigaidi. LAkini serikali ya Ufaransa ilibaini kuwa yote yanawezekana.

■ Mabaki ya MS804 bado kupatikana

"Mabaki yaliyogunduliwa sio yale ya ndege yetu", naibu kiongozi wa EgyptAir Ahmed Adel amesema kwenye runinga ya CNN. Bw Adel alirejelea kauli aliyoitoa kwenyeruninga ya Marekani kwa kutangaza kugunduliwa kwa mabaki ya ndege ya EgyptAir.

Mapema jioni, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wa Anga nchini Ugiriki alikanusha tangazo la kiongozi washirika la ndege la Misri la EgyptAir. "Hadi sasa, tathmini ya mabaki yaliogunduliwa inabaini kwamba sio ya ndege ya shirika l andege la EgyptAir, " Athanassios Binos amesema.

→ SOMA ZAIDI: Misri bado yajiuliza chanzo cha ajali ya ndege ya EgyptAir

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.