Pata taarifa kuu
KENYA-UJANGILI

Pembe za ndovu kuchomwa moto Ijumaa

Maelfu ya pembe za ndovu zilizonaswa nchini Kenya zitateketezwa moto kesho jijini Nairobi mbele ya marais kadhaa wa bara la Afrika.

Pembe za ndovu zilizokamatwa nchini Kenya. Ujangili umeongezeka katika nchi hii.
Pembe za ndovu zilizokamatwa nchini Kenya. Ujangili umeongezeka katika nchi hii. Harambee Kenya
Matangazo ya kibiashara

Uchomaji wa pembe hizo utaongozwa na rais Uhuru Kenyatta akiwa na marais wengine wa bara la Afrika kutoka Botswana, Gabon, Kenya na Uganda watakaokutana kujadili namna ya kumaliza uwindaji haramu wa ndovu barani Afrika.

Inaelezea kuwa Tani 120 za pembe hizo za ndovu ndizo zitakazoharibiwa kuashiria vita dhidi ya uwindaji huo haramu.

Viongozi hao wa Afrika wanatarajiwa kutumia mkutano utakaofanyika mjini Nanyuki kutangaza mikakati mipya dhidi ya uwindaji wa ndovu katika mataifa yao.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kuhifadhi Wanyamapori nchini humo (KWS) Kitili Mbathi, amesema Kenya haiamini kuwa pembe hizo zina thamani yoyote na hivyo itaendelea na mpango wa kuziteketeza.

Watalaam wa kuhifadhi wanyamapori wanaonya kuwa ikiwa mauaji haya yataendelea, huenda ndovu watakatoweka barani Afrika kwa sababu wanyama hao wapatao elfu 30 huuawa kila mwaka.

Nchini Tanzania, mwaka 2009 ilikuwa na ndovu 110,000 na kufikia mwaka 2014 walikuwa wamesalia 43,000 tu idadi ambayo inaendeela kupungua kwa sabbau ya uwindahu haramu.

Ndovu wakitembea katika tambarare kilomita 220 kusini mwa mji wa Nairobi, Kenya.
Ndovu wakitembea katika tambarare kilomita 220 kusini mwa mji wa Nairobi, Kenya. AFP PHOTO / TONY KARUMBA

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.