Pata taarifa kuu
Caracas-Mzungumzo

Papa Francis awataka wanasiasa nchini Venezuela kumaliza tofauti zao

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amewatolea wito viongozi wa nchini Venezuela pamoja na upinzani kuwa na moyo wa kishujaa wakati huu wakianza mazungumzo ya kutafuta suluhu ya kumaliza maandamano yasio koma, ikiwa ndio njia moja pekee ya kupatikana muafaka.

Papa Francis Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani.
Papa Francis Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani. REUTERS/Tony Gentile
Matangazo ya kibiashara

Papa Francis ameweka bayana hii leo Ijumaa ujumbe wake ambao ulisomwa jana jijini Caracas na muakilishi wake Aldo Giordano mbele ya pande zinazo zozana wakati pande hizo zilipo kutana kwa mara ya kwanza katika mazungumzo.

Ujumbe huo unawalenga rais Nicolas Maduro, wajumbe wa serikali, pamoja na wawakilishi wa muungano wa upinzani pamoja na wajumbe wa muungano wa nchi za Amerika ya kusini wanaosiumamia mazungumzo hayo.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakati wa mkutano na Upinzani April 7, 2014.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro wakati wa mkutano na Upinzani April 7, 2014. REUTERS/Miraflores Palace

Serikali ya kisocialist nchini Venezuela ilikuwa imeomba Pietro Parolin muakilishi wa zamani wa kiongozi wa kanisa katoliki nchini humo kusimamia mazungumzo hayo, ombi ambalo halikujibiwa moja kwa moja na Papa Francis, lakini tayari Vatican inawakilishwa kwenye mazungumzo hayo na muakilishi wake jijini Caracas.

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro pamoja na viongozi wa upinzani licha ya kubadilisha maneno makali kwenye mazungumzo yaliyorushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni nchini humo, bado pande hizo mbili zimeshindwa kuafikiana.

Hali ilikuwa tete zaidi, wakati upinzani ulipoweka mezani dai lake la kwanza ili kufikia suluhu na Serikali, na kwamba wanataka kuachiwa kwa wafungwa wote waliokamatwa wakati wa maandamano ya kuupinga utawala wake jambo ambapo rais Maduro alikataa na kupuuzilia mbali.

Kiongozi wa Upinzani Henrique Capriles wakati wa mazungumzo na Nicolas Maduro,  Caracas, April 10, 2014.
Kiongozi wa Upinzani Henrique Capriles wakati wa mazungumzo na Nicolas Maduro, Caracas, April 10, 2014. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins

Wakati wa mkutano wa leo, rais Maduro ameyatuhumu baadhi ya maiundi ya upinzani kwa kupandikiza chuki nchini humo pamoja na kutaka kuipindua Serikali, tuhuma ambazo pia upinzani umezipuuza.

Mazungumzo mengine yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne ambapo mpaka sasa raia 40 wameshauawa toka kuanza kwa maandamano ya kupinga mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha toka kuingia madarakani kwa rais Maduro.

Mazungumzo hayo yanalenga kumaliza vurugu za maandamano yalioshuhudiwa kwa kipindi cha miezi miwili iliopita kudai usalama bora na uboreshwaji wa hali ya maisha kwa wananchi wa taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.