Pata taarifa kuu
URUSI-MAREKANI-UKRAINE-Diplomasia

Urusi yainyooshea Marekani kidole cha lawama

Urusi imeituhumu Marekani kuzuia shughuli za Taasisi ya uangalizi wa usalama na ushirikiano wa bara ulaya OSCE Mashariki mwa Ukraine wakati huu mapigano yakijiri katika eneo la ajali ya ndege ya MH17 na kukwamisha juhudi za kimataifa za kuimarisha usalama katika eneo hilo.

Vladimir Putin akinyooshea Marekani kidole cha lawama.
Vladimir Putin akinyooshea Marekani kidole cha lawama. REUTERS/Michael Klimentyev
Matangazo ya kibiashara

Wazirini wa Marekani mwenye dhamana ya mambo ya nje, John Kerry (kusoto), akiwa pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov (kulia).
Wazirini wa Marekani mwenye dhamana ya mambo ya nje, John Kerry (kusoto), akiwa pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov (kulia). REUTERS/Carolyn Kaster

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, kupitia mazungumzo kwa njia ya simu amemuomba waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry kuwaamuru maafisa wa marekani kuacha kuwazuia OSCE kufanya shughuli zake.

Katika mazungumzo hayo waziri wa marekani John Kerry ameitaka Urusi kuanza utekelezaji wa kusitisha mapigano, ameeleza afisa mmoja wa ikulu ya marekani.

Kutokana na mapigano Taasisi ya uangalizi wa usalama na ushirikiano wa bara la Ulaya wamekuwa wakikwama kufanya shughuli zao hasa kukaribia eneo la ajali ya ndege ya Malaysia Airlines, ambayo ilitokea zaidi ya majuma mawili yaliyopita na kuua watu 298.

Kwa upande wa wachunguzi kutoka Uholanzi na Australia zimeeleza hii leo kuwa hakuna uwezekano wa kukaribia eneo la ajali, jitihada zitahitaji muda kutokana na mapigano katika eneo hilo.

Eneo ambako mabaki ya ndege yaMalaysia Airlines yaliyodondokea, katika mji wa Donetsk, Julai 17..
Eneo ambako mabaki ya ndege yaMalaysia Airlines yaliyodondokea, katika mji wa Donetsk, Julai 17.. Reuters/Maxim Zmeyev

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umetoa ripoti, ambamo umelani utumiaji wa silaha kali katika maeneo yanayokaliwa na raia wa kawaida mashariki mwa Ukraine. Umoja wa Mataifa umewanyooshea kidole waasi wa Ukraine pamoja na jeshi la nchi hiyo. Umoja wa Mataifa umebaini kwamba zaidi ya watu 1.100 wameuawa katika mapigano mashariki mwa Ukraine tangu yalipoanza katikati mwa mwezi wa Aprili.

 

“watu takribani 1.129 wameuawa, na wengine 3.442 wamejeruhiwa, tangu jeshi la Ukraine lianzishe operesheni dhidi ya ugaidi, katikati ya mwezi wa Aprili, kulingana na takwimu za Julai 26 mwaka 2014, umoja wa Mataifa, umethibitisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.