Marekani : mji wa Ferguson waendelea kukumbwa na machafuko
Hali ya sintofahamu inaendelea kutanda katika mji wa Ferguson (Missouri) kufuatia maandamano yenye misingi ya rangi, amabyo yamesababisha watu wawili kujeruhiwa usiku wa jumatatu kuamkia jumanne wiki hii, huku watu 31 wakiwa wamekamatwa.
Imechapishwa:
Hivi karibuni rais wa Marekani Barack Obama, alitoa wito wa kukomesha maandamano hayo, akiitaka polisi kutotumia nguvu kwa kuwatawanya waandamanaji.
Mji huo mdogo ulioko katikati ya Marekani unakabiliwa na machafuko tangu askari polisi alipomuua kijana mweusi, Michael Brown, Agosti 9 katika mazingira ya kutatanisha.
Polisi imesema watu wawili wamejeruhiwa kwa risase ziliyofyatuliwa na waandamanaji.
“Wahanga wamejeruhiwa kwa risase ziliyopigwa kutokea upande wa waandamanaji”, mkuu wa polisi, Ron Johnson, ameambia vyombo vya habari, huku akibaini kwamba rais Obama ameitaka polisi kutotumia nguvu, na ndiyo maana polisi haijafyatua risase, na imetumia mabomu ya kutoa machozi katika dakika ya mwisho, baada ya kuona kwamba waandamanaji wameanza kutumia silaha za moto.
Johnson amesema kwamba askari polisi wanne wamejeruhiwa kwa mawe yaliyorushwa na waandamanaji, huku akibaini kwamba baadhi ya waandamanaji 200 ambao wamekua wakirusha mawe ni kutoka jimbo la New York na California.