Pata taarifa kuu

Washington yajiandaa kushambulia Dola la Kiislam, Moscow yaonya

Saa 24 baada ya rais wa Marekani, Barack Obama kuhutubia taifa lake kuhusu uwezekano wa kushambulia Dola la Kiislam, mjadala umeibuka kuhusu kuingilia kijeshi nchi ya Syria.

REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hadi sasa washirika wa Marekani wako tayari kuendesha mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa kiislam nchini Iraq, lakini kuvuka mpaka hadi Syria limekua ni suala gumu, huku ikulu ya washington ikishindwa kutoa uamzi kuhusu operesheni hiyo dhidi ya Dola ya Marekani.

Suala lingine ambalo limeibua mjadala ni kuhusu kusaidia upinzani bila hata hivo kuutambua kwa mara nyingne uhalali wa utaewala wa Bashar Al Assad. Washauri wa Barack Obama wamelihakikisha suala hili kufuatia kauli walizotoa hivi karibuni ambazo zinafanana na kauli ya Baracka Obama : “ Marekani haitosita kuwashambulia wapiganaji wa kiislam licha ya kuwa watapatikana upande wa pili wa mpaka hususan nchini Syria. Hii ni operesheni ambayo imeshapangwa”.

Hata hivo, iwapo Barack Obama na washirika wake waako tayari kushambulia wapiganaji wa kiislam nchini Iraq, itamlazimu rais huyo wa Marekani kuwasilisha kwenye bunge la Congress pendekezo la kuwasaidia kijeshi waasi wa Syria kutokana na sababu za kibajeti. Wakati huohuo baadhi ya wabunge kutoka chama cha Conservative wamebaini kwamba kuna ulazima pendekezo hilo liwasilishwe bungeni ili lipigiwe kura. Wabunge wametofautiana kuhusu pendekezo la kuingilia kijeshi nchini Syria.

Hayo yakijiri Urusi kupitia waziri wake wa mambo yanje, Sergueï Lavrov amesema kuingilia kijeshi aidha kushambulia wapiganaji wa kiislam nchini Syria itakua ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa kwa kuingilia kijeshi taifa bila idhni ya utawala wa taifa hilo. Hayo ni wakati mashambulizi ya anga yanayoendeshwa na jeshi la Marekani dhidi ya wapiganaji wa kiislam nchini Iraq yameungwa mkono na serikali ya Baghdad.
“ Iwapo Marekani inataka kushambulia wapiganaji wa kiislam nchini Syria inatakiwa ipewe idhni na Utawala wa rais Bashar Al Assad ili kujilinda kukiuka sheria za kimataifa”, Sergueï Lavrov, amesema.

Waziri Lavrov amekumbusha alhamisi kwamba Iwapo Marekani itashambuliwa wapiganaji wa kiislam nchini Syria bila idhni ya Umoja wa Mataifa na utawala wa Serikali halali ya Damas itakua ni uchokozi dhidi ya Urusi.

Tangu ulipoanza mgogoro wa Syria, Urusi imekua ikiunga mkono utawala wa Bashar Al Assad na kuzuia uamzi wa mataifa ya magharibi ambayo yalikua yakijaribu bila mafaanikio kuuchukulia vikwazo utawala wa Bashar Al Assad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.