Pata taarifa kuu
MAREKANI-ISRAEL

Marekani yatiwa wasiwasi na amri ya kuendeleza ujenzi katika eneo la mashariki mwa Jerusalem

Rais wa Marekani Barrack Obama amekutana jana na waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu na kumwambia kuhusu wasiwasi wa Marekani juu ya uamuzi wa Israel kuanza ujenzi wa maakazi mapya ya walowezi wakiyahudi eneo la Mashariki mwa Jerusalem.

Benyamin Netanyahu, akipokelewa Ikulu ya Marekani na rais Barack Obama
Benyamin Netanyahu, akipokelewa Ikulu ya Marekani na rais Barack Obama REUTERS/Jason Reed
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya viongozi hao wawili kukutana katika mazungumzo ya ana kwa ana, Waziri Mkuu Netanyahu aliendelea kusisitiza Iran kuzuiliwa kuendelea na mpango wake wa Nyuklia na Marekani kuendela kusadia upatikanaji wa amani Mashariki ya Kati.

Mkutano huo wa ana kwa ana kwenye Ikulu ya rais ya Marekani kati ya Rais Obama na waziri mkuu wa Israel ni wa kwanza kufanyika tangu kumalkizika hivi karibuni kwa mapigano kati ya Israel na Kundi la Hamas mjini Gaza, yaliogharimu maisha ya watu 2.100 upande wa Palestina na zaidi ya 70 upane wa Israel.

Marekani inaguswa zaidi na taarifa za kutowa idhini ya ujenzi wa makaazi mapya 2.610 mashariki mwa Jerusalem, ambapo swala hilo limejadiliwa na viongozi hao wawili katika ofisi ya rais Obama.

Marekani inasema ikiwa ujenzi huo utaendelea Mashariki mwa mji huo unaowaniwa kati ya Israeli na Palestina, huu utakiwa ni ujumbe mzito kwa Palestina, na huenda kukashudiwa mapigano mapya kati ya pande hizo mbili, jambo ambalo inafaa kuliepuka.

Kuendeleza shughuli za ujenzi katika eneo hilo, kunadhohofisha juhudi zote za kutafuta amani kati ya Israel na Palestina. Manispaa ya jiji la Jerusalem iliruhusu mradi huo wa ujenzi tangu Desemba 2012, laskini iliwekwa kando tangu kipindi hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.