Pata taarifa kuu
BRAZIL-Uchaguzi-Siasa

Brazil: Dilma Rousseff aongoza katika uchaguzi

Kulingana na matokeo ya mwisho, rais anayemaliza muda wake, Dilma Rousseff amechukua nafasi ya kwanza katika duru ya kwanza ya uchaguzi nchini Brazil, akiongoza kwa pasenti kubwa dhidi ya washindani wake Aecio Neves na Marina Silva ambaye ni mwanamazingira.

Dilma Rousseff baada ya kupiga kura, Jumapili Oktoba 5 mwaka 2014, katika mji wa Porto Alegre.
Dilma Rousseff baada ya kupiga kura, Jumapili Oktoba 5 mwaka 2014, katika mji wa Porto Alegre. REUTERS/Paulo Whitaker
Matangazo ya kibiashara

Aecio Neves amepata asilimia 33.68 ya kura huku Marina Silva akipata asilimia 21.29 ya kura.

Marina Silva amewondolewa katika kinyanganiro hicho cha kugombea kwenye kiti cha rais, jambo ambalo limewashangaza wengi katika duru ya kwanza ya uchaguzi. Hivi karibuni mwanamazingira huyo alipewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo, baada ya utafiti wa kwanza kuonesha kuwa anaungwa mkono na idadi kubwa ya raia, lakini matokeo ya mwisho ya uchaguzi yameonesha kuwa Marina Silva amepata asilimia 21.29 ya kura.

Takribani asilimia 99 ya kura zimehesabiwa. Duru ya pili ya uchaguzi itakayofanyika Oktoba 26 mwaka 2014, itawakutanisha Aecio Neves na Dilma Rousseff. Ambaye ni rais anaye maliza muda wake.

Rais Dilma Rousseff amepata asilimia 41.48 ya kura, huku Aecio Neves akipata asilimia 33.68.

Aecio Neves, ambaye ni mgombea kwenye uchaguzi wa rais kwa tiketi ya chama cha kisoshalisti amefaulu kuchukua nafasi ya pili na kumshinda Marina Silva, ambaye alikua akipewa nafasi kubwa ya kushinda duru ya kwanza ya uchaguzi.

Marina Silva alichukua nafasi ya Edouado Campos ya kugombea kwenye kiti cha rais baada ya kifo chake kiliyotokana na ajali ya ndege mwezi Agosti.

Kwa upande wake rais anaye maliza muda wake Dilma Rousseff amewaambia wafuasi wake kwamba pambano linaendelea.

“ Kwa mara nyingine tena raia wa Brazil wamekuana na imanai na mimi katika duru hii ya kwanza ya uchaguzi. Ninazidi kupongeza ushirikiano wa rais wa zamani Lula, bila yeye siningeweza kufika hapa nilipo, na kutekeleza ndoto yangu ya kuiendeleza Brazil katika sekta mbalimbali. Kwa hiyo pambano linaendelea”, amesema rais Dilma Rousseff akiwaambia wafuasi wake.

Hata hivo, vyombo vya habari nchini Brazil vimekua vikieleza uwezekano wa mazungumzo kati ya Aecio Nevez na Marina Silva kwa minajili ya kumuangusha Dilma Rousseff.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.